KINANA ATAKA MADHEHEBU YASHIKAMANE KUDUMISHA AMANI


KATIBU Mkuu wa CCM,Abdalrahman Kinana,amesema mshikamano wa Watanzania utadumu iwapo Madhehebu yote ya Dini yatashikamana na kuchangia amani na umoja wa nchi yetu.

Pia Kinana aliwataka na kuwahimiza waumini wa dini zote, wenye uwezo bila kujali itikadi zao kisiasa na kidini, wamkumbuke Mwenyezi Mungu awawezeshe nao wawasaidie wasio nacho.

Kinana alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza, wakati Futari iliyoandaliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Wilaya ya Tarime,Omar Mwita Gachuma kwa ajili ya Waumini wa Kiislamu hapa.
“Nimshukuru Omar Gachuma kwa kunialika kushiriki jambo hili la kheri.Mwaka jana alinialika sikuja,mwaka huu karudia na kusema lazima uje.”

“Ndugu zangu hii ndiyo Tanzania tunayoitaka na ndiyo tunayoiju,ambayo watu wa itikadi zote na dini zote, wenye tofauti wanakusanyika pamoja katika mema na majonzi.Mshikamano wa Tanzania utadumu madhehebu yote yatakaposhikama kama hivi tulivyo hapa,”alisema Kinana

Katibu Mkuu huyo wa CCM alisema “wenye uwezo mkumbukeni Mwenyezi Mungu awawezeshe, muwakumbe wasio  na uwezo.Ni vizuri akikupa uwasaidie wasio na uwezo.Tumwoombe Mungu atukubalie saumu zetu.”

Awali Gachuma,kushiriki kula futari hiyo kunaondoa kuhitilafiana kwa dini na kijamii,hivyo ni jambo jema kushiriki na kutukutana pamoja.
“Ndugu zangu futari hii inatukutanisha pamoja na kutuondolea kuhitilafiana kwa dini zote.Inatuunganisha watu wa dini zote.Mimi naitwa Omar Gachuma, nimefunga na nimepunguza kilo 5 tangu mwezi huu uanze ,”alisema Omar Gachuma .

Alisema Kinana anajitahidi kujenga usawa na katika nchi yetu,hivyo wamwombee kwa ssababu bado aana muda mrefu wa kufanya shughuli za taifa letu.

Aidha Mkuu wa mkoa Evarist Ndikilo,alisema kwaa kutukutanisha watu wa dini na itikadi mbalimbali,hivyoWaumini wa dini ya Kiislamu wautumie mfungo wa mwezi Ramadhani kuuombea mkoa wa Mwanza,sababu una mchango mkubwa wa amani ya nchi yetu.

Alisema futari hiyo ni ya nane na imekuwa ikiandaliwa na Mjumbe wa NEC (CCM) , Omar Gachuma  kwa ajili ya ndugu zetu Waislamu na si kila mtu anaweza kufanya hivyo kutokana na majukumu yake.
“Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Kinana nikushukuru kwa kutenga muda wako kuja kujumuika na ndugu zetu Waislamu kufuturu nao pamoja.Nimshukuru pia Omar Gachuma,ni mara yake ya 8 akiandaa futari,”

“Nitumie fursa hii kukuomba, ninayo makundi mbalimbali ya wajasiriamali,unisaidie walau kundi moja na nitakuwa  nimefaidika sana,maana wako bega kwa bega na serikali katika kujiletea maendeleo,”alisema Ndikilo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI