MALKIA NOMSA MATSEBULA WA SWAZILAND AZURU TANZANIA KWA MWALIKO WA MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE

IMG_5607Malkia wa Swaziland Mheshimwa Nomsa Matsebula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Ndugu Nurdin Babu mara baada ya helikopta iliyomchukua kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati huko wilayani Rufiji ambako alikwenda kutembelea Shule ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA. Tarehe 2.7.2014. Kulia ni Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.
IMG_5611Mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland Malkia Nomsa Matsebula akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wamanakayama Dkt. Ramadhan Dau mara baada ya mgeni huyo kuwasili huko Nyamisati tarehe 2.7.2014.
IMG_5621 Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwa amefuatana na mwenyeji wa Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamisati waliofika kumlaki mara baada ya helikopta iliyomleta kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati tarehe 2.7.2014.

IMG_5653 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akimshuhudia Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Shule ya Sekonadri  Wamanakayama.
IMG_5673Mwanafunzi Assia Idd akimwonyesha Malkia Matsebula kutoka Swaziland namna ya kutumia i-pad kwenye masomo ya sayansi na hesabu wakati Malkia huyo alipotembele Shule ya Sekondari ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
IMG_5718Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akipanda mti wa kumbukumbu ya kutembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Wamanakayama iliyoko katika Kijiji cha Nyamisati katika wilaya ya Rufiji.
IMG_5892Mke wa Mama Salma Kikwete akimpokea Mgeni wake Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula mbele ya jengo la ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA.IMG_5974Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake zawadi ya picha.

PICHA NA JOHN LUKUWI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI