MBUNGE KABATI AKAGUA MIRADI ILIYOZINDULIWA NA MWENGE

 Mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati kulia akikagua choo  cha soko la Kitwiru soko ambalo   limekimbiwa na wafanyabiashara baada ya kukosa umeme (picha na Francis Godwin Blog)
Diwani wa kata ya  Kitwiru katika Manispaa ya Iringa Ally Mbata wa  pili  kulia akimwonyesha  mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) jiwe la msingi ambalo  liliwekwa na kiongozi wa mbio za mwengi Kitaifa mwaka 2012 wakati wa uzinduzi wa  soko la Kitwiru ambalo kwa zaidi ya mwaka mmoja  sasa  halitumiki kutokana na kukosa umeme soko hilo limejengwa kwa zaidi ya Tsh milioni 22 (picha na Francis Godwin Blog)

 
MBUNGE wa  viti maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) ameanza ziara ya kukagua miradi mbali  mbali katika  jimbo la Iringa ikiwa ni  pamoja na kulitembelea  soko lilolozinduliwa na mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 ambalo wafanyabiashara  wamelihama  kutokana na kukosekama kwa  huduma ya umeme .


Soko   hilo  lililopo  eneo la kata ya Kitwiru  katika Manispaa ya  Iringa awali  lilikuwa  likitumiwa vema kabla ya mambo ya siasa  kuingizwa  kwa wafanyabiashara kuhamasishwa kuhama eneo hilo na kwenda  kufanya biashara  yao eneo la Mashine tatu badala ya kwenda  katika  soko  hilo la kisasa  kwa madani ni porini.

Akiwa katika ziara  hiyo jana  sokoni hapo  diwani wa kata ya  Kitwiru Ally Mbata  alimweleza  mbunge Kabati kuwa  soko hilo  lilijengwa kwa ajili ya  kuwawezesha wafanyabiashara   wa  kata ya  Kitwiru  kupata  eneo la kufanyia biashara  pia  wananchi kupata  soko kwa ajili ya kununua mahitaji mbali mbali.

Hata   hivyo  alisema  soko  hilo ambalo lilifahamika kama gulio la kata ya Kitwiru  lilikuwa  likifanay kazi  vizuri na uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa  uliboresha  zaidi kwa kupeleka  huduma ya maji na vyoo  vya kisasa ila tatizo lililopelekea  wafanyabiashara  kuhama ni umeme  kutokana na soko  hilo lilikuwa  likifanya kazi kila jumapili kuanzia mchana hadi jioni  pekee.

Mbata  alisema  ili  soko  hilo liweze  kufikiwa na huduma ya umeme ni nguzo tatu   pekee  ndizo  zinazohitajika kufikisha umeme  katika  soko  hilo .

Aidha  alisema soko  hilo  iwapo  lingeboreshwa kwa  kuwekwa  umeme  lilikuwa ni kitega uchimi  kikubwa kwa kata hiyo ya Kitwiru japo alisema  upo mkakati wa kulifufua  soko  hilo.

Kwa upande wake  mbunge Kabati alisema kuwa  lengo la ziara  yake  hiyo katika soko  hilo na maeneo mengine imelinga kuangalia  utekelezaji wa ilani ya chama  cha mapinduzi (CCM) na kuona miradi ambayo  inaanzishwa  inaendelezwa kwa kiasi gani .

Alisema ataendelea  kufanya ziara  katika miradi mbali mbali ili  kuona usimamizi wa miradi hiyo na ile lenye changamoto kama  huo  basi kuangalia uwezekano wa kuiendeleza kwa faida ya  wananchi ambao  ni wahitaji wa  miradi hiyo ya kimaendeleo .

Mbunge kabati  alisema kuwa soko  hilo la Kitwiru  iwapo  lingeendelezwa  lilikuwa na faida  kubwa  kwa vijana na  wanawake ambao   wageweza  kupata ajira  zaidi katika  soko  hilo kwa kufanya biashara mbali mbali ila  kuendelea kubaki pasipo  kutumika kwa  soko hilo ni hasara kubwa kwa serikali hasa  ukizingatia kiasi kikubwa cha fedha  zilizotumika katika ujenzi wa soko  hilo .
MWISHO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*