MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA KUFANYA MAMBO JIMBO LA CHALINZE, SAFARI HII NI ZAMU YA JESHI LA POLISI

              

1A
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya ulizni na usalama wa raia na mali zao. Pamoja na kukabidhi kompyuta hizo zitakazosaidia katika utunzaji wa kumbukumbu pia mbunge huyo ametoa fedha  kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya Mbwewe na Kiwangwa ambavyo  thamani inafikia zaidi ya shilingi milioni 11, Kushoto kwake ni Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani  ACP Ulrich Onesphory Matei, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana kwenye kituo kikuu cha polisi Chalinze.
1
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S. Magomi.
2
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.
3
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.
4
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete  akimsikiliza Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa niaba ya jeshi la polisi mkoani Pwani mara baada ya kukabidhiwa kompyuta hizo , katikati ni mkuu wa  ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
5
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee Bw. Kamis Kameza wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa shule hiyo ambayo inajengwa na jeshi la kujenga taifa JKT kambi ya Ruvu.
6
Baadhi ya wanajeshi wa kambi ya JKT Ruvu wanaoshiriki katika ujenzi wa shule hiyo.
7
Moja ya madarasa ya shule hiyo ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wake.
8
Baadhi ya madarasa na maktaba ya shule hiyo yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake.
9
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete  akisalimiana na wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee wakati alipokagua ujenzi wa shule hiyo.
10
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kufanya ukaguzi wa ujenzi shuleni hapo kushoto ni Diwania wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser.
11
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikweteakikagua ujenzi wa Maktaba ya shule hiyo akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Bwilingu Ahmed Nasser mbele na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Khamis Kameza.
12
Baadhi ya wananchi waliohudhuria wakati wa hafla  kukabidhi kompyuta kituo cha polisi Chalinze.
13
Diwani wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser akizungumza wakati mbune wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipolokabidhi jeshi la polisi kompyuta kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*