MKUU WA MKOA WA DODOMA DK. NCHIMBI AZINDUA UJENZI WA BARABARA MAYAMAYA DODOMA HADI BABATI

 Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi Dereva Abuu Ally Funguo ya kuwashia mitambo ya kujengea barabara kuashiria kuanza rasmi kwa Ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zilizofanyika mapema jana Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo Wilayani Kondoa,Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini Mhe. Zabein Mhita.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (Katikati mwenye kilemba) na ujumbe alioambatana nao wakipatiwa maelezo ya mradi wa barabara kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kutoka kwa wakandarasi wa Kampuni inayojenga barabara hiyo ya China Railway Seventh Group wakati
alipotembelea kambi ya kampuni hiyo  iliyopo kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa mapema jana Julai Mosi, 2014.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe alioambatana nao wakikagua magari yanayotumika kwenye ujenzi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami Mapema jana wakati wa maadhimisho ya kusherehekea kuanza kwa ujenzi wa mradi huoyaliyofanyika Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa, wengine pichani ni wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara hiyo kipande cha Bonga-Mela (88.8KM).

 Wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu ya Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani) wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huozilizofanyika Jana Julai Mosi, 2014 kwenye Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa.

 Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa waliojitokeza kwa wingi kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani), Sherehe hizo zilifanyika
mapema Jana Julai Mosi, 2014.




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wadau, Mafundi na Wataalamu wa Kampuni ya China
Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi
Bonga Babati kwa kiwango cha lami kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) wakiwa
kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuanza
kwa ujenzi wa mradi huo wa barabara zilizofanyika Kijijini Kolo Wilayani
Kondoa Mapema Jana Julai Mosi, 2014. PICHA ZOTE NA MDAU JOHN BANDA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA