Rais Dkt. Jakaya Kikwete aendelea na ziara Namtumbo


      
D92A7268Mtoto Gloria Fusi mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Utwango wilayani Namtumbo akiandika jina lake katika Notebook ya Mama Salma Kikwete wakati Rais Kikwete aliposimama katika kijiji cha Utwango kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mjini Namtumbo akitokea Songea mjini. Mtoto Gloria alimsalimia Mama Kikwete kwa uchangamfu na ndipo Mama Salma alipomuuliza kama anajua kuandika jina lake na hivyo kumpatia notebook yake na mtoto huyo bila kusita aliandika vizuri jina lake.
D92A8180Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Mzee Mustafa Mangunyuka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa taifa wilayani Namtumbo ambapo aliwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.
D92A8301Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mbunge wa Namtumbo Mh. Vita Kawawa muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuwahutubia mamia ya wakazi wa Namtumbo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa taifa mjini Namtumbo.
D92A8357 D92A8345Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia mamia ya wakazi wa Namtumbo katika uwanja wa taifa mjini Namtumbo leo.
D92A8357Mamia ya Wakazi wa Namtumbo waliohidhuria mkutano wa hadhara ulihutubiwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika uwanja wa taifa mjini Namtumbo (picha na Freddy Maro).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*