Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na wasanii kutoka nchini Marekani

               

jk1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto) na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
jk2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto) na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
jk3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
jk12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na wasanii hao.
……………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu Julai 14, 2014 amekutana na kundi la wasanii kutoka Marekani lililowasili nchini usiku wa Alhamisi, Julai 10, 2014, kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa wasanii wa Tanzania kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mjini Dar es Salaam.
Wasanii hao ni pamoja na Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group.
Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Kiasi cha wasanii 250 walishiriki semina hiyo inayoitwa Mafunzo ya Uendelezaji Usanii. Hiyo ilikuwa ni kutimiza ahadi aliyotoa Rais Kikwete kwa wasanii wa Tanzania kuwa atachangia kuinua kiwango cha ujuzi na weledi wao kwa kuwaandalia mafunzo yatayoendeshwa na magwiji wa sanaa kutoka Marekani sasa imetimia.
Akizindua Kampeni ya Uzalendo kwa Vijana inayoendeshwa na Muungano wa Wasanii Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwezi uliopita, Juni 14, 2014, Rais Kikwete aliahidi kuchangia kuinua kiwango cha usanii na weledi wa wasanii wa Tanzania kwa kusaidia kuandaa mafunzo yatakayoendeshwa na wasanii maarufu kutoka Marekani.
Mbali na kuendesha shughuli za mafunzo ya wasanii ambazo wamekuwa wakizifanya kwa makundi madogo madogo tokea walipowasili nchini, pia wanamuziki hao wa Marekani na kundi la wapiga picha watatembelea sehemu mbali mbali nchini, hasa kwenye vivutio vya watalii, ambako watapiga picha na kuandaa vipindi vya kuitangaza Tanzania katika vyombo vya habari vya Marekani.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Julai,2014

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI