TPDC yatoa ufafanuzi kuhusiana na mkataba wake na Statoil

      

PIX 1Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania.
PIX 2Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Andilile (kushoto) akijibu maswali toka kwa waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano uliohusu Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari zilizokinzana kuhusu Kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane.
PIX 3PIX 4 PIX 5Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo wakifuatilia kwa makini taarifa ya ufafanuzi iliyokuwa ikitolewa na baadhi ya Viongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Na Benedict Liwenga na Winner Abraham-MAELEZO.
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC limetoa ufafanuzi kuhusiana na Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari zilizokinzana kuhusu Kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane ameeleza taarifa zilizo sahihi kuhusu kampuni ya Statoil na mikataba yake  mbalimbali na Serikali katika upataji wa faida kutokana na utafutaji wa  mafuta na gesi .
Killagane ameeleza kuwa utaratibu unaotumika katika kutafuta mafuta ni aghali sana na ni hatari kwa maisha, hivyo serikali haiwezi yenyewe kuingia gharama hizo za utafutaji na badala yake inatumia mifumo mbalimbali kama vile Concession agreement, Service agreement pamoja na Mkataba wa kugawana mapato ambapo kati ya mikataba hiyo mitatu Serikali inatumia mkataba wa kugawana mapato ambapo humpa mwekezaji kazi kisha rasilimali zikigunduliwa hugawana na kampuni hiyo au mwekezaji aliyegundua. Hivyo serikali inategemea kupata mrahaba na kodi toka kwa makampuni inayoingianayo mikataba.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi amevieleza vyombo vya habari kuwa ugunduzi wa gesi unategemea miundo mbinu mingi sana na inategemea uwingi wa gesi hiyo ndiyo maana serikali inaingia mikataba na makampuni makubwa yenye uwezo mkubwa wa kifedha ili kuweza kufanya utafiti na kuchimba mafuta na gesi.
Aidha, Bw. Killigane amefafanua kuwa mkataba walioingia kati ya Serikali na kampuni ya Statoil mwaka 2007 ulikuwa ni wa kutafuta mafuta na sio gesi lakini hapo mwaka 2012 mkataba mwingine wa kutafuta gesi ulifanyika kati ya kampuni hiyo na Serikali.
“Statoil ilipendekeza kuwa kwenye mgao wa mkataba wa mwanzo serikali ipate asilimia 5% statoil asilimia 95% kama zabuni iliyokuwa imeletwa, lakini baadaye kamati ikakaa na kuzungumza na mwekezaji ambapo mwekezaji aliweza kusukumwa kutoka asilimia 5% hadi asilimia 30% na hivyo hii ilijumuisha TPDC kuweza kujiunga kwa asilimia 10%, kwa sasa katika mkataba wa mafuta serikali inapata asilimia 56% na Statoil asilimia 44%, katika mkataba wa wagesi serikali inapata asilimia 61% na mwekezaji asilimia 39% katika kipindi cha mkataba”. Alisema Killigane.
Naye Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Andilile aliwahakikisha waandishi wa habari kuwa serikali iko tayari kusaidiana na waandishi wa habari katika kutoa taarifa sahihi ili kuweza kuwaeleza watanzania kuhusiana na sekta ya mafuta na gesi na nini kinaendelea.
“Hii nchi ni yetu na kazi zote tunazozifanya ni kwajili ya watanzania, jinsi waandishi wa habari wanavyotoa taaarifa zisizo sahihi wanaharibu sura ya nchi yetu na kuwapa hofu wawekezaji na hivyo kuleta hasara badala ya faida, kama kuna jambo lisiloeleweka tunawaomba kwa wakati wowote mkituita tutakuwa tayari kuwapa taarifa ili wote kuwa katika ufahamu mmoja”. Alisema Andilile.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU