Vifo zaidi ya 600 vimetokana na Ebola huko Afrika
Magharibi.
Shirika la Afya Duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu
wanaofariki kutokana na mkurupuko wa maradhi ya Ebola katika maeneo ya Afrika
magharibi, sasa imepanda na kufikia zaidi ya watu 600.
Yamkini watu wengine 68 wamefariki katika kipindi cha juma moja
lililopita.
Maofisa wa matibabu wa kimataifa na wale wa maeneo hayo wanajaribu kuyafikia
maeneo ya mataifa yaliyothirika na ugonjwa huo kama vile Guinea, Sierra Leone na
Liberia.
Changamoto zachelesha udhibiti wa Ebola Afrika
Magharibi
Uvumi, wasiwasi,imani potovu na kutoaminiana kunachochea kusambaa kwa ugonjwa
huo huku baadhi ya wanaviji huenda wangali wanawaficha wagonjwa wao kwa hofu ya
kutengwa.
Ebola ni ugonjwa hatari unaosambaa kwa kasi mno hivyo huenda idadi kamili ya
vifo vinavyotokana na Ebola isijulikane.
Baadhi ya waliowahi matibabu sahihi mapema wamepona.
Comments