VIONGOZI WA TANZANIA WAENDA KUJIFUNZA SINGAPORE


 Baahi ya mitaa ya nchini Singapore iliyotembelewa na viongozi waandamiizi wa serikali ya Tanzania walioko nchini humo kwa mafunzo. Nchi ya singapore ni miongoni mwa nchi zenye majengo marefu duniani

 Viongozi waandamizi wa serikali ya tanzania wakipata maelezo kuhusu uendeshaji wa bandari ya Singapore ambayo imepata mafanikio makubwa kwa kuhudumia makontena milioni 32 kwa mwaka, mafanikio ambayo yametokana na uendeshaji wa huduma hiyo kwa ubia na serikali chini ya mfumo wa PPP.
Baadhi ya makatibu wakuu wa wizara mbalimbali za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baadhi ya watendaji wakuu wa mashirika ya umma walioko kwenye ziara ya mafunzo nchini Singapore iliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania, hapa wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao ambao ni taasisi ya kimataifa ya biashara ya Singapore, Internatioanal Enterprise Singapore
Mtaalam wa bandari ya Singapore, Wan chee Foong akitoa maelezo kwa ujumbe wa Tanzania uliko kwenye mafunzo nchini humo akieleza kuhusu namna bora ambayo imeiwezeza Singapore kuhudumia makontena milioni 30 kwa mwaka ikilinganishwa na Tanzania ambayo inahudumia makontena laki sita tu 9picha na Vedasto Msungu)

Na Vedasto Msungu, Singapore

Makatibu wakuu wa baadhi ya wizara katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadhi ya watendaji wakuu wa mashirika ya umma wako nchini Nsingapore kwa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi, UONGOZI INSTITUTE ya Tanzania.

Akiongea nchini Singapore, kiongozi wa ujumbe wa makatibu wakuu hao, Dk Frolens Turuka ambae ni Katibu mkuu ofisi ya Waziri mkuu amesema ziara hiyo ya viongozi waandamizi wa serikali inalenga kujifunza kuhusu mfumo wa uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa kushikisha sekta binafsi chini ya mfumo wa PPP (Public Private Partnership).

Dk Turuka amesema mfumo huo umeisaidia sana nchi ya Singapore kupiga hatua kubwa kimaendeleo tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1965 na ikaanza kuwekeza katika teknolojia na biashara ya kimataifa.

Amesema Tanzania kupitia taasisi ya Uongozi ambayo imekuwa ikiandaa mafunzo ya aina mbalimbali kwa viongozi, inachukua mfumo huo kama mfano wa PPP kuigwa ambao unaweza kuisaidia nchi kupiga hatua kubwa za kiuchumi na kijamii.

Aidha Dk Turuka amesema licha ya kuwa nchi hii ya Singapore ni ndogo ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 716 tu lakini ina maendeleo makubwa ambayo hayafanani na nchi nchi duniani zenye rasilimali nyingi za kiuchumi ikiwemo Tanzania.

Hata hivyo amesema mfumo chini ya mpango wa mapokeo makubwa sasa unaotekelezwa na serikali ya Tanzania na ushirikiano kati ya sekta binafsi, anayo imani kwamba nchi itapata mafanikio makubwa.

Nae Denis Rweyemamu kutoka taasisi ya Uongozi, inayoratibu ziara ya mafunzo kwa viongozi hao amesema hii siyo mara ya kwanza kwa Uongozi Institute kuandaa mafunzo kama hayo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali.

Amesema taasisi hiyo itaendelea kuandaa mafunzo kama hayo kwa viongozi mafunzo yanayolenga kusaidia kuharakisha maendeleo ya Tanzania kijamii na kiuchumi chini ya mfumo wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa ubia kati ya serikali na sekta binafsi.

Pamoja na Katibu Mkuu ofisi ya waziri mkuu Dk Frolens Turuka, wengine waliomo kwenye ziara hiyo ya mafunzo nchini Singapore ni Katibu Mkuu wizara ya Fedha Dr Servacius Likwelile, Katibu Mtendaji tume ya Mipango, Ofisi ya rais Dk Philip Mpango, Katibu mkuu wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, Katibu Mkuu wizara ya Maji, Injinia Bashir Mrindoko, Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali, George Masaju na Dk Shaban Mwinjaka, Katibu mkuu wizara ya Uchukuzi.

Wengine ni Injinia Joseph Nyamhanga, Naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi, Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme nchini TANESCO injia Felichesmi Mramba, Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,TPA injinia Madeni Kipande, Kamishina wa PPP, wizara ya Fedha, Dk Frank Mhilu, Mkuu wa Idara ya utafiti na sera kutoka taasisi ya Uongozi, Denis Rweyemamu, Amir Said kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania TIC na Linda Manu kutoka taasisi ya Uongozi

Wakiwa nchini Singapore, ujumbe huu wa viongozi waandamizi wa serikali ya Tanzania na watendaji wakuu wa mashirika ya umma, wanatembelea taasisi mbalimbali za sekta binafsi ambazo zinatekeleza majukumu mbalimbali ya kwa ubia kati ya serikali ya Singapore na sekta binafsi katika maeneo ya usafiri, Bandari, maji, nishati usafirishaji.

Ziara hiyo kwa nchini Singapore inaratibiwa na taasisi ya kimataifa ya biashara ya serikali ya Singapore iitwayo International Enteprise Singapore- IES.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*