Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson akiwa na shost yake Wema Isaac Sepetu.
KAMA hakuwahi
kutoa sadaka, huu ndiyo muda wake! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt
Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu
baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a
Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Habari
zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo lilijiri Jumapili
iliyopita nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha
tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la
Mwengi Ally.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana, Mwengi
alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo timbwili
lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.
Ilidaiwa
kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka wasichana
saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua kwamba
katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake, angeumizwa
Aunt alikimbilia nyumbani kwa shoga yake, Wema.
Ilidaiwa
kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza Aunt hadi
wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini walikutana na
meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man ambaye
walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali na
waume za watu.
Ilisemekana
kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na msichana wake
aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia wasichana hao
kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani
yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye hadi mkewe
akanasa meseji zao za mapenzi.
Baada ya
kujazwa data hizo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwengi ili kupata
maelezo ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda kwa Aunt na
Wema lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama angemkamata, maafa
yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na Aunt maeneo ya
Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto akamfanyie shopping.
Alisema
baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni kama mama
yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni Diamond,
kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine kimejificha.“Niliporudi
nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa kutumia simu yake,
nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.
“Nilipoisoma
ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu kuhusu mapenzi
yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani kwake
nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha kwa
jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za watu,”
alisema Mwengi.
Alipotafutwa
Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi: “Sina muda
mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.”
Comments