AZAM FC YATUMA KIKOSI CHA UBINGWA KAGAME, WAHAITI WOTE NDANI...MWAIKIMBA NA DIARA NJE


AZAM FC  imetuma kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame michuano inayoanza wikiendi hii mjini Kigali, Rwanda.
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiengua Yanga SC katika michuano ya Kombe la Kagame na nafasi hiyo kupewa Azam FC, zote za Tanzania.
Yanga SC imeenguliwa kwa sababu moja tu kubwa, kushindwa kuthibitisha kupeleka kikosi cha kwanza pamoja na kocha Mkuu, Marcio Maximo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.
Azam FC imetuma kikosi cha wachezaji 20 Kombe la Kagame

Yanga SC ilitakiwa hadi jana jioni kuwa imethibitisha na kutuma kikosi, lakini haikufanya hivyo na CECAFA ikawasiliana na TFF kuwaambia wapeleke timu nyingine iliyo tayari na zali likawaangukia Azam FC.
Yanga SC ilitaka kupeleka kikosi cha vijana kwenye nashindano hayo, jambo ambalo CECAFA waliwakatalia wakiwaambia hiyo si michuano ya watoto.
Kikosi ambacho Azam FC wametuma Kigali ni makipa; Aishi Manula, Mwadini Ally, mabeki Waziri Salum, Gadiel Michael, Shomary Kapombe, Abdallah Kheri, Aggrey Morris, Said Mourad na David Mwantika.
Viungo Kipre Balou kutoka Ivory Coast, Salum Abubakar, Mudathir Yahya, Himid Mao, Khamis Mcha ‘Vialli’, Farid Mussa na Joseph Peterson wa Haiti, wakati washambuliaji ni Mrundi Didier Kavumbangu, Leonel Saint- Preux wa Haiti, Kipre Herman Tchetche wa Ivory Coast na John Bocco ‘Adebayor’.
Mshambuliaji kutoka Mali, Ismaila Diara na mkongwe Gaudence Mwaikimba hawamo kwenye kikosi hicho kitachoongozwa na kocha Mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog, Msaidizi Kali Ongala, kocha wa makipa Iddi Abubakar na Meneja, Jemadari Said.  
Azam FC, mabingwa wa Tanzania Bara, sasa wanaingia Kundi A katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame ya 40 pamoja na wenyeji, Rayon Sport, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de L’Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti wakati Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
Timu 14 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo kuanzia Agosti 8 hadi 24 mwaka huu- jumla ya mechi 34 zikichezwa katika viwanja vya Amahoro na Nyamirambo, Kigali. 
Azam itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya wenyeji Rayon Sport Uwanja wa Amahoro Agosti 8, mwaka huu, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya 
KMKM ya Zanzibar na Atlabara ya Sudan Kusini. 
Azam FC itarudi tena dimbani, Agosti 10 kumenyana na jirani zao KMKM, kabla ya kucheza na Atlabara Agosti 12 na kukamilisha mechi za kundi lake, kwa kumenyana na Coffee ya Ethiopia Agosti 16.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU