DIAMOND AMCHEFUA WEMA

KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.
Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan

kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa Kitanzania wala Kiafrika.
Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai-sound vizuri na pengine haiwezekani kwa mwanamke kulazimisha kuolewa kama mwanaume hataki. Hicho ndicho kilichomtibua Madam (Wema) baada ya kusoma alichokisema Diamond

kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Wema amehisi yeye ni girl lover (mpenzi) tu kwa Diamond na si wife material (mke mwema) kwa hiyo  anawaza sana kuhusiana na ishu hiyo japo mahaba niue kati yao yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua uamuzi mzito.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta mlimbwende huyo anayeshikilia Krauni ya Miss Tanzania 2006 ili kumsikia mwenyewe ambapo alifunguka yake ya moyoni.
Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa haumizi tena kichwa kuhusu  suala la ndoa na Diamond na kwamba hana haraka nalo.
Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha anioe.
Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu (Diamond).
Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi
alisema Wema.
Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu (Diamond).
Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi
alisema Wema.
Paparazi wetu alimtwangia simu mama yake Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza mambo mawili, kuhusu bintiye kuvishwa pete ya ndoa na Diamond na suala la Mbongo Fleva huyo kusema hataoa kamwe!
Mimi niseme nini? Sina la kusema kuhusu Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini mnipigie mimi, si mumtafute yeye mwenyewe?
alisema mama huyo kwa sauti ya utulivu.
Katika hali ya kushangaza, mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana kunawa mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za nyuma kuhusu mtoto wake na masuala ya kutooa au kuoa.
Nasibu ni mtu mzima sasa, siwezi kumpangia lolote kuhusu kuoa au kutooa. Wakati ukifika, anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri katika maisha yake.
Kuhusu Diamond kumvisha pete ya ndoa Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni wakiwa nchini Afrika Kusini,
shehe mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake ambapo alisema alichokifanya Diamond kwa Wema ni usanii.
Diamond amemfanyia usanii mwenzake. Pete gani bila kufunga ndoa. Halafu katika Uislam, hakuna tendo la wanandoa kuvalishana pete, hayo mambo wanayafanya wenyewe
alisema shehe huyo.
Wema alipopewa nafasi ya kuizungumzia pete hiyo alisema Diamond aliipenda tu akaamua kumnunulia na kumvisha lakini haihusiani na ndoa.
Sisi (na Diamond) tulikuwa Afrika Kusini, baby wangu akaipenda pete, akainunua na kunivalisha, haina uhusiano na ndoa
alisema Wema

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU