FIGO NA MAGWIJI WENZAKE REAL MADRID WAANDALIWA MAPOKEZI ‘BAAB KUBWA’ WAKITUA DAR KUWAVAA AKINA PAWASA, LUNYAMILA


Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MAPOKEZI makubwa yameandaliwa kwa ajili ya kikosi cha magwiji wa klabu ya Real Madrid kitakachotua nchini Agosti 22, kwa ziara ya siku kadhaa ikiwa ni pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki.
Mkurugenzi wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), Farough Baghozah ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba magwiji hao watapokewa kwa maandamano Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kupelekwa hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach.
“Tumeandaa mapokenzi mazuri yenye hadhi ya kimataifa, wageni watapokewa kwa maandamano ya aina yake na kupelekwa katika hoteli ya Ladger Plaza Bahari Beach,”amesema Baghozah ‘Master’.
Mmoja wa Waratibu wa zoara ya Real Madrid nchini, Said Tuliy kulia akiwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Real Madrid, Royco Garcia katika kikao juzi mjini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa TSN, Farough 'Master' Baghozah kushoto akiwa na Royco Garcia

Aidha, Baghozah amesema tayari kikosi cha magwiji wa Tanzania, kitakachomenyana na Real Madrid kimeanza mazoezi Uwanja wa Karume kwa ajili ya mchezo.
“Tunatarajia sana tukio hili la kipekee Tanzania litafana na tunaomba sana wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya mchezo (Agosti 23,) Uwanja wa Taifa ili kuwaoa heshima yao magawiji hawa,”amesema.
Baghozah amesema kwamba Tanzania inakuwa nchi pekee barani Afrika kupata fursa hii ya kuupokea ugeni huo mzito wa Real Madrid hivyo ni tukio la kujivunia na itakuwa vyema watu wakijitokeza kwa wingi siku hiyo.   
Makipa maarufu waliowahi kuwika nchini, Mwameja Mohamed na Manyika Peter wamejumuishwa katika kikosi cha Tanzania All Stars kitakachomenyana na magwiji hao wa Real Madrid. 
Chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa kikosi hicho kitaingia kambini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo huo wa Agosti 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Wengine walioItwa ni mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, 
Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo, 
Viungo Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda. 
Wanakuja; Magwiji wa Real Madrid, Figo na Zidane wanatarajiwa kuwamo katika msafara 

Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Real Madrid watakuja nchini Agosti 22.
Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.
Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
Kampuni ya Vodacom Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara pamoja na Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Wito umetolewa kwa makampuni zaidi kujitokeza kudhamini ziara hiyo ya kihistoria nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI