MTIBWA, POLISI MORO KUCHEZA MECHI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Timu
za Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zinazojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) zitacheza Jumamosi (Agosti 23 mwaka huu) mechi ya majaribio ya
mfumo wa tiketi za elektroniki.
Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa 10 jioni wakati kiingilio kitakuwa sh. 1,000.
Tiketi
za mechi hiyo zitaanza kuuzwa kesho (Agosti 20 mwaka huu) kupitia
mtandao wa M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma
yaliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, wengi wao wakiwa
Morogoro Mjini.
Washabiki 100 wa kwanza kuingia uwanjani wapata jezi za timu za Mtibwa Sugar na Polisi.
Tayari
mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki imeshafanyika kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu za Tanzania Prisons
na Mbeya City zilipambana na kutoka sare.
Mechi
nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zitachezwa Agosti 30
mwaka huu. Uwanja wa Mkwakwani jijini utakuwa na mechi kati ya Coastal
Union na Mgambo Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni
Kagera Sugar dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.
Septemba
6 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na
Mtibwa Sugar. Mechi nyingine ni ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga
itakayofanyika Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
*WAAMUZI KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI
Waamuzi
wanaotarajia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu watafanya mtihani wa utimamu wa mwili
(physical fitness test) mwezi ujao.
Mtihani
huo utahusisha waamuzi wa daraja la kwanza (class one) wakiwemo pia
wale wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Mbali
ya mtihani huo unaotarajiwa kufanyika kabla ya Septemba 10 mwaka huu,
pia kutakuwa na semina kwa makamishna ambao watasimamia mechi za VPL na
FDL.
Hivyo waamuzi wote wanatakiwa kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi kwa ajili ya mtihani huo.
*MAKOCHA COPA COCA-COLA KUNOLEWA DAR
Makocha
wa kombaini za mikoa zitakazoshiriki Copa Coca-Cola mwaka 2014 pamoja
na waamuzi vijana wa michuano hiyo watashiriki kozi ya ukocha na uamuzi
itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu.
Kozi
hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka
huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya
Taifa itakayochezwa Septemba mwaka huu.
Makocha
watakaoshiriki kozi hiyo na mikoa yao kwenye mabano ni Ahmed Simba
(Mwanza), Ally Kagire (Kagera), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma
(Tabora), Anthony Mwamlima (Mbeya), Athuman Kairo (Morogoro), Bakari Ali
(Kaskazini Pemba) na Charles Mayaya (Shinyanga).
Fidelis
Kalinga (Iringa), Gabriel Gunda (Singida), Hafidh Muhidin Mcha (Kusini
Pemba), Hamis Mabo (Kigoma), John William (Geita), Joseph Assey
(Shinyanga), Joseph Haley (Manyara), Jumanne Ntambi (Kilimanjaro),
Leonard Jima (Ruvuma), Madenge Omari (Mara), Mohamed Muya (Dodoma),
Nicholas Kiondo (Ilala) na Nurdin Gogola (Temeke).
Osuri
Kosuli (Simiyu), Peter Amas (Arusha), Ramadhan Abdulrahman Ramadhan
(Mjini Magharibi), Renatus Mayunga (Kinondoni), Samwel Moja (Lindi),
Seif Bakari (Katavi), Shaweji Nawanda (Mtwara), Sheha Khamis Rashid
(Kaskazini Unguja), Tigana Lukinjo (Njombe), Yusuf Ramadhan Hamis
(Kusini Unguja), Zahoro Mohamed (Tanga) na Zakaria Mgambwa (Rukwa).
Waamuzi
vijana watakaoshiriki kozi hiyo chini ya Mkufunzi wa FIFA, Felix
Tangawarima wa Zimbabwe ni 33. Kwa upande wa ukocha Mkufunzi ni Ulric
Mathiott kutoka Shelisheli.
*KOZI YA UKOCHA LESENI A KUFANYIKA SEPTEMBA 4
Kozi
ya ukocha wa Leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) itafanyika mara ya kwanza nchini, jijini Dar es Salaam
kuanzia Septemba 4 mwaka huu.
Mkufunzi
wa kozi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume atatoka CAF,
na itamalizika Septemba 8 mwaka huu wakati ada ya ushiriki ni sh.
300,000.
Washiriki
wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B ya ukocha ya CAF. Fomu kwa ajili ya
ushiriki wa kozi hiyo zinapatikana kwenye ofisi za TFF na tovuti ya
TFF.
Comments