KAULI YA DIAMOND PLATNUM KUHUSIANA NA SERENGETI FIESTA 2014 MKOANI MWANZA.


Mkali wa Mziki wa Kizazi Kipya hapa Bongo Diamond Platnum aka Rais wa Wasafi aka Dangote aka mahaba ninyote wa Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 tayari yuko Jijini Mwanza kwa ajili ya amsha amsha za Serengeti Fiesta 2014 ambayo inakata Utepe hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Akipiga Story ndani ya 99.4 Metro FM ya Jijini Mwanza hii leo, Platnum amebainisha kuwa kwa mara ya Kwanza atashusha burudani kali kwa wapenda burudani wa Mkoa wa Mwanza na Vitongoji vyake ikiwa ni katika Kufungua Msimu Mpya wa Serengeti Fiesta 2014 kwa mara ya Kwanza kabisa ikiwa inaanzia Kanda ya Ziwa ndani ya Mkoani MwanzaAmesema kuwa siku zote alikuwa akipanda jukwaani na madancers wane, lakini hii leo kwa mara ya kwanza atapanda jukwaaani na madancers 10 na atatumbuiza ngoma yake ambayo amesema inafanya poa sana katika ardhi ya Bongo kwa hivi sasa, ngoma ya mdogo mdogo.

Akizungumzia ngoma hiyo ya mdogo mdogo, Diamond amesema kuwa imemuongezea heshima kubwa hapa bongo kwa kuwa ndiyo ngoma ambayo inapendwa zaidi kwa hivi sasa kati ya ngoma zake, japo ameongeza kuwa inje ya bongo inayotamba sana kwa hivi sasa ni ile aliyofanya na Iyanya ambayo inafahamika kama Bum Bum.
Tayari homa ya Serengeti Fiesta 2014 Mkoani Mwanza imeishaanza kunoga na Milango tayari imefunguliwa ambapo wasanii wakali wa Mwanza wataanza amsha amsha za Serengeti Fiesta 2014 kuanzia majira ya saa 11 za jioni kabla ya mastaa kibao kuonyesha makeke yao.Kumbuka Kiingilio ni shilingi 5,000 tu, kiukweli hii si ya kukosa. Kumbuka Platnum pia anatarajiwa kuwa na Mrembo wake katika Show hiyo ambapo pia Wema Tayari yuko ndani ya Jijini la Mwanza.
Platnaum akishow love na Watangazaji wa Metro FM.
Serengeti Fiesta 2014 Mkoani Mwanza, Ni Sheeeeeda....Sambaza Upendo.
Na: Georege Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.