KIFO CHA MAKAMU WA BLATTER, MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI FIFA



GRONDORA
Rais wa Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.

Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).
Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya Fifa na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*