MAKALLA AKAGUA UJENZI WA BWAWA KUBWA LA MAJI CHOLE, WILAYANI KISARAWE

 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akizungumza baada ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa vijiji vya Chole na Kwala, wilayani Kisarawe mkoani Pwani leo. Bwawa hilo linalotarajia kukamilika mwezi ujao ambalo limejengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 1.5, litakuwa na uwezo wa kutoa lita milioni 250 kwa mwaka. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Selemani Jaffo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Makalla akikagua ujenzi wa bwawa hilo la Chole
 Bwawa la Chole linalojengwa na kampuni ya kitanzania ya Kika
 Makalla akikagua kisima kipya cha Kimani wilayani Kisarawe
Wananchi wakiangalia wakati Naibu Waziri wa Maji, Makalla, akipampu maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Mengo, wilayani Kisarawe.
Makalla akimtwisha ndoo ya maji Zena Mwinyihija baada ya kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mengo, wilayani Kisarawe.
Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Jaffo baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Chole, wilayani Kisarawe.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Makalla akihutubia baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Tanki la maji katika Kijiji cha Chole.
Naibu Waziri Amos Makalla  akisaidiwa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Jaffo kufunua pazia wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tanki la Maji katika Kijiji cha Chole. Tanki hilo liltakuwa linahifadhi maji kutoka bwawa kubwa litakalokuwa linahifadhi maji ya mvua.
Katibu wa Bodi ya Maji ya Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe, Pwani, Fatuma Chambuso akisoma taarifa ya usimamizi wa mradi wa maji uliozinduliwa na Naibu Waziri wa Maji katika Kijiji hicho
Wananchi wa Kijiji cha Chakenge wakifurahia uzinduzi wa mradi wa maji kijijini hapo
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chakenge, Mohamed Ndege akimkabidhi zawadi ya mbuzi Naibu Waziri Makalla.
Wananchi wa Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe wakicheza muziki wa Mweanamuziki Naseeb Abdul 'Diamond Platinamuz' wakifurahia kuzinduliwa kwa mradi wa maji uliofanywa na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akiungana na wananchi kucheza muziki mpya mdogo mdogo wa Mwanamuziki Diamond, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe, Pwani. PICHA ZOTE NAN KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU