MBINU YA KUSAKA MTOTO !!! HAYA NDIYO YANAYOFAA KUZINGATIA ILI KUSHIKA MIMBA KIURAHISI.

Zingatia mambo haya sasa

Mayai ya mwanamke ni mojawapo ya viungo ambavyo vimeshatengenezwa kabla hata mwanamke hajazaliwa, yaani tangia akiwa fetus ndani ya tumbo la mama yake.


Haya mayai yanakuwa tayari pale msichana anapopata menstruation yake ya kwanza average ya miaka 12 hadi 14. 



Kuanzia hapo hadi pale atakapofikia menopause/kikomo cha menstruation kwa mwanamke (average miaka 51) mayai yake na fertility yake hupungua anavyozidi kuzeeka.
Yaani katika ujana wake, teenage na 20s ni muda ambao ni rahisi zaidi kutunga mimba. Na kuanzia miaka 30 had 51 uwezo huu unapungua kwa kiasi kikubwa mpaka unapoisha kabisaa.

Wakati kwa wanaume wao sperm cell zinaanza kutengenezwa pale wanapo balehe(puberty age) mpaka siku atakayo kufa. Hii inamaanisha kama mwanaume akiwa katika hali nzuri ya kiafya anaweza kumpa mimba mwanamke hadi afikapo uzeeni iwapo mwanamke bado hajafikia menopoase na ni fertile.


Moja, Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwiilini.

Pili, Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kuathairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
 
  Tatu, Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)
Nne, Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanamme.

Tano, Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanamume aweze kuboreshe na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio.
Sita, Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.
Saba, Jiepushe kunywa kahawa na vinywaji vinginevyo vyenye caffeine. Waataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.
Nane, Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.
 
Tisa, Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. 


Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume. Kumi, Hakisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. http://www.manyandahealthy.com

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI