TAMKO LA IKULU KUHUSU MSIMAMO WA UKAWA

KURUGENZI ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema Rais Jakaya Kikwete hana mamlaka ya kusitisha Bunge Maalumu la Katiba kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Bw.Salva Rweyemamu, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Bw. Rweyemamu alikuwa akikanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki ambalo liliandika habari iliyobeba kichwa cha habari “Rais Baraka Obama amgeuka JK”.
Alisema Rais Kikwete hana mamlaka ya kusitisha Bunge hilo kwani Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haijampa mamlaka hayo hivyo ni vyema watu wakaisoma sheria hiyo na kuielewa.
Aliongeza kuwa, sheria hiyo haitoi nafasi kwa mtu mwingine kulivunja Bunge hilo bali tofauti zilizopo watazimaliza wenyewe akiwataka wajumbe wa Bunge hilo waliosusia vikao kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), warejee bungeni kuendelea na vikao ili wananchi wapate Katiba Mpya.

Akizungumzia taarifa iliyoandikwa na gazeti hilo, alisema habari hiyo haina ukweli bali imetungwa kwani katika mkutano uliofanyika Mjini Washington D.C, nchini Marekani hivi karibuni, masuala hayo hayajazungumzwa kama inavyodaiwa. 
Habari hii ilikuwa ikisema Rais Barack Obama wa Marekani amemuuliza Rais Kikwete kuhusu fedha za Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL zilizochukuliwa kutoka Benki Kuu nchini (BoT)
alisema.
Alisema katika mkutano uliowakutanisha viongozi mbalimbali, hakuna jambo la IPTL ambalo lilizungumzwa ambapo Rais Kikwete alikutana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Misaada la Maendeleo nchini Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Aliongeza kuwa, Rais Kikwete pia alizungumza na Rais wa Malawi, Peter Mutharika ambaye alimkaribisha nchini kwake ili wakale samaki wa ziwa Malawi linalojulikana kama ziwa Nyasa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*