UONAPO DALILI HIZI ZA EBOLA WAHI KITUO CHA AFYA MAPEMA, SOMA HII NA SAMBAZA KWA WENZAKO

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA
Mnamo mwezi wa Machi 2014 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi ambao ulianzia katika ya Guinea na kusambaa katika nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Hadi tarehe 31 Julai, 2014 idadi ya wagonjwa ilikuwa 1323 na vifo 729.

Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi.
Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa:
o kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo
o kugusa maiti wakati ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu.
o kugusa wanyama walioambukizwa Mizoga na wazima kama vile sokwe na swala wa msitu.
Aidha Ugonjwa wa Ebola hauna tiba wala chanjo.
Hadi sasa hapa nchini Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa virusi vya Ebola.
Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii imeandaa mikakati ya kuzuia ugojnwa huu usiingie hapa nchini na ikiwa utaiingia uweze kudhibitiwa kabla haujasambaa. Mikakati hiyo ni pamoja na:
o Kuunda kikosi kazi (Task Force) kinachohusisha wajumbe mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na WHO, UNICEF, USAID na CDC kwa ajili ya kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu ikwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa mpango wa dharura wa kukabiliana na Ebola ambao tayari umeandaliwa.
o Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Makatibu Tawala na Waganga Wakuu wote wa Mikoa. Aidha taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli, na na namna ya kuwahudumia wagonjwa. 
o Kuboresha ufuatiliaji na utambuzi wa ugonjwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na mipakani ili kuweza kubaini wasafiri watakaoonyesha dalili za ugonjwa au wenye viashiria hatari. .
o Miongozo ya utoaji elimu imeandaliwa ikiwemo Vipeperushi. Aidha watalaamu wa Afya wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili endapo ugonjwa huo ukitokea uweze kutolewa taarifa mapema
o Vifaa kinga (Personal Protective Gears) vipo vya kutosha na Wizara imeanza kuvisambaza kutoka bohari za kanda za MSD na kuzipeleka kwenye vituo vya kutoa huduma za afya ili watumishi wa afya waweze kutumia iwapo mgonjwa atajitokeza. Aidha idadi itaongezwa kadiri ya mahitaji yatakavyojitokeza.
o Wizara imebainisha vituo vya kutolea huduma kwa mikoa yote iwapo endapo ugonjwa huu utatokea hapa nchini. Aidha katika vituo hivi, vifaa kinga pamoja na madawa vimeshaandaliwa.
o Kuwasiliana na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo ili kuweza kupata msaada wa mahitaji mbalimbali kama yalivyoainishwa kwenye mpango wa dharura wa kukabliana na Ebola ulioandaliwa.
Hitimisho
Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu ila kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu. Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika. Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu ni:-
o Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola
o Wananchi wanatahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
o Wananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola.
o Zingatia usafi wa mwili tabia na kiroho.
o &bbsp; Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola.
o Kuwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu.
Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali kuimarisha ufuatiliaji ili kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI