WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI JUU WALIFADHILIWA NA TBL WAPATA MAVUNO MENGI

 Mkulima (wa pili kulia) wa Shayiri katika mashamba ya Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha akiendelea na uvunaji wa Shayiri kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wameweza kuvuna hadi gunia 1o kwa hekari moja. Wakulima wa Monduli Juu wameanza kuvuna mazao yao, baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) iliyowapatia mafunzo, mikopo ya mbolea na dawa. Pia shayiri hiyo hununuliwa na TBL kwa ajili ya kutengenezea kimea katika kiwanda kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

 Afisa Ugani wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Monduli Juu na West Kilimanjaro, Editha Temu akipima kuangalia ubora wa Shayiri iliyoanza kuvunwa katika mashamba ya Monduli Juu. Kushoto ni  ni Mwenyekiti wa wakulima wa Shayiri Monduli Juu Bariki Kivuyo.

 Mkulima wa Shayiri Goigoi Kivuyo akionyesha sehemu ya shamba linalotarajiwa kuvunwa Shayiri eneo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha, baada ya kulima kwa kufuata maelekezo na mkopo  wa mbegu na dawa kutoka Kampuni ya TBL
: Mkulima wa mfano Mepoloo Lolosi aliyelima hekari 180 za Shayiri katika eneo la Monduli Juu wilayani Monduli, mkulima huyo alikuwa akionyesha baadhi ya zana za kilimo ambazo aliwezeshwa kuzipata kwa njia ya mkopo ili kufikia malengo yake ya kulima kisasa.  Tayari amekwisha kumaliza kuzilipia zana hizo pamoja na nyingine.
Meneja wa Barley kutoka  Kiwanda cha Bia nchini (TBL) Dk. Bennie Basson akiwaonyesha waandishi wa habari hawao pichani namna Kampuni hiyo inavyowawezesha wakulima wa Shayiri katika kulima kilimo bora chenye tija.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI