habari mpasukooo!!!!! AJALI NYINGINE MBAYA YA BASI LA AIRBUS YATOKEA GAIRO

 
Habari za hivi punde kutoka Mkoani Morogoro zinapasha kuwa basi la Kampuni ya Airbus lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda Tabora limepata ajali muda si mrefu eneo la Kiegeya Wilayani Gairo Mkoani Morogoro.
Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Faustine Shilogile ameiambia Father Kidevu Blog kuwa ni kweli kuna ajali nae yupo eneo la tukio.
"Ninaomba unitafute baade kidogo kwa taarifa kamili kwa sasa nipo eneo la ajali huku Gairo," alisema SACP Shilogile.
 Father Kidevu Blog itakujuza zaidi kuhusiana na tukio hilo ambalo linaelezwa kugharimu uhai wa watu 4 papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*