HISPANIA YAIFUMUA MACEDONIA 5-1 KUFUZU EURO


HISPANIA imefufua makali, baada ya kuanza vyema kampeni za kufuzu Euro 2016 kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Macedonia.
Kocha Vincente Del Bosque alianzisha wachezaji wanane waliokuwepo kwenye Euro 2012 na Sergio Ramos akafunga bao la kwanza kwa panalti dakika ya 16 baada ya David Silva kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Paco Alcacer akafunga la pili dakika ya 17 baada ya kazi nzuri ya Juanfran kumpiga chenga kipa. Juanfran akawapa wapinzani penalti iliyofungwa na Agim Ibraimi dakika ya 28 aliyemtungua vizuri Iker Casillas.

Mwanzo mzuri: David Silva akiwa amemrukia mgongoni Paco Alcacer kushangilia naye bao la pili mjini Valencia jana

Sergio Busquets akafunga bao la tatu dakika ya 45 na ushei, kabla ya Silva kufunga la nne dakika ya 50 na Pedro kufunga la tano dakika ya 90 na ushei. Silva sasa amefikisha mabao mengi zaidi kwa wachezaji ambao si washambuliaji kihistoria Hispania, mbali na Fernando Hierro. 
Kikosi cha Hispania kilikuwa: Casillas; Alba, Abidol, Ramos/Bartra dk68, Juanfran, Busquets, Silva, Koke/Munir dk77, Fabregas, Pedro na Alcacer/Isco dk57.
Macedonia: Pacovski, Cuculi, Sikov, Mosjsov, Alioski/Demiri dk46, Trajkovski, Spirovski/Radeski dk64, Ristovski, Abdurahimi/Velkoski dk74, Jahovic na Ibraimi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU