JENGO LENYE OFISI ZA UBALOZI YA MAREKANI LATEKWA NA WANAMGAMBO LIBYA.

Mwanachama wa kundi la Down of Libya akiwa ndani ya jengo la mazoezi kwenye eneo la ubalozi wa Marekani, Libya  Aug. 31, 2014.
Mwanachama wa kundi la Down of Libya akiwa ndani ya jengo la mazoezi kwenye eneo la ubalozi wa Marekani, Libya Aug. 31, 2014.

Kundi moja la wanamgambo wa ki-Islam nchini Libya linasema limechukua udhibiti wa eneo la makazi yaliyoachwa wazi na ubalozi wa Marekani mjini Tripoli mwezi mmoja baada ya wanadiplomasia wa Marekani kukimbia ghasia za mapambano kati ya wanamgambo hasimu katika mji mkuu wa Libya.

Mashirika ya habari yaliripoti jumapili kwamba kundi la Dawn of Libya, kundi mwamvuli la wanamgambo wa ki-Islam lilisema linadhibiti eneo la Marekani kwa wiki moja na walilichukua eneo hilo kutoka kwa kundi moja la wanamgambo hasimu baada ya wiki kadhaa za mapigano ili kuwania udhibiti wa Tripoli na uwanja wake wa ndege wa kimataifa.

Mtandao wa televisheni wa Al Arabiya wenye makao yake Dubai ulirusha hewani video moja inayoonesha wanamgambo wapiganaji wakiruka kutoka kwenye paa na kuingia kwenye bwawa la kuogelea kwenye eneo la Marekani. Balozi wa Marekani kwa Libya, Deborah Jones alisema video hiyo inaonekana kuchukuliwa katika eneo la makazi ya ubalozi. Alisema ubalozi unaonekana kuwa salama na sio kushambuliwa.

Wawakilishi wa Marekani walikimbilia nchi jirani ya Tunisia mwishoni mwa mwezi Julai ili kuepuka mapambano mjini Tripoli huku Marekani inasema itasitisha kwa muda operesheni zake za ubalozi hadi hali ya usalama iwe shwari.

Ghasia zinaongezeka nchini Libya katika muda wa miaka mitatu tangu alipoondolewa diktekta wa muda mrefu nchini humo Moammar Gadhafi. Wakati huo huo baraza la wawakilishi la upinzani, moja lililopo mjini Tripoli na jingine lililopo umbali wa kilomita 1,500 huko Tobruk wamemchagua waziri mkuu wao kuongoza nchi.http://www.voaswahili.com

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*