KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MAFIA , ASAFIRI NA ABIRIA WA KAWAIDA KATIKA BOTI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda kwenye boto katika Bandari ya Mafia kwenda Bandari ya Nyamisati, wilayani Rufiji baada kufanya ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la ofisi ya CCM Wilaya ya Rufiji. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mafia, Abdulkarim Shaha.
 Kinana akifunua pazia wakati wa uzinduzi wa jengo hilo la kisasa.
 Kinana na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo hilo
 Kinana akiondoka baada ya kuzindua jengo hilo
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akisikiliza hotuba ya Kinana huku akiwa amesimama juu ya stuli wakati Kinana alipokwenda kukagua ujenzi wa tuta la kuzuia mafuriko ya bahari katika Vijiji vya Jimbo,Banja na Jojo wilayani Mafia
 Kinana, Nape na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao wakikagua tuta hilo
 Kinana akitoka kukagua ujenzi wa mradi wa maji wa bomba la Visiwa vya Chole na Juani wilayani Mafia
 Kinana akiangalia Kisiwa cha Chole alipokuwa akikagua mradi wa bomba la maji la visiwa vya Chole na Juani
 Kinana akiangalia korongo linaloathiri Uwanja wa Ndenge wa Mafia
 Green Guard wa CCM wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana
 Kinana (katikati) akiwa na viongozi wengine wa CCM alipokuwa akikagua ujenzi wa gati la Mafia lililozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka jana.
 Kinana akipatiwa zawadi la sanamu ya Boti na Katibu wa CCM Wilaya ya Mafia wakati wa hafla ya kumuaga bandarini Mafia.
 Kinana akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza ndani bodi iliyokuwa inatoka Mafia kwenda wilayanio Rufiji
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akizungumza na wana CCM ndani ya Boti katika msafara wa Kinana.
 Kinana akiwa amejichanganya na abiria wengine ndani boti akisafiri kutoka Mafia kwenda Bandari ya Nyamisani wilayani Rufiji
 Mkuu wa Mawasiliano wa CCM, Chongolo (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya abiria ndani ya boti hilo
 Baadhi ya waandishi wa habari walio kwenye msafara wa Kinana wakiwa ndani ya boti hiyo ya abiria wa kawaida
 Kinana na msafara wake ukiteremka kwenye boti katika Bandari ya Nyamisati kutoka Mafia
Nape akiwa na viongozi wa CCM pamoja na abiria alipokuwa akiteremka kwenye boti katika Bandari ya Nyamisati wilayani Rufiji

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.