NHIF YAKAMATA WATU WANAOTUMIA KADI ZA BIMA YA AFYA KINYUME NA UTARATIBU KATIKA HOSPITALI YA REGENCY


1Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es salaam. Baada ya kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kutumia kadi ya bima ya afya yenye namba 02-HCTP1801 ambayo inamilikiwa na Bw. Terry J. Maona kinyume na utaratibu , Mtu huyo alikamatwa jana katika hospitali hiyo wakati akitaka kufanya vipimo vya (CityScan), ndipo mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo alipogundua na kupiga simu makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwataarifu kuhusiana na tukio hilo, ambapo maofisa walifika na kukamata nyaraka hizo huku mgonjwa akitokomea kusikojulikana baada ya kugundulika, Bw. Julius Mziray amewaasa wamiliki wa kadi za Bima ya Afya kutozitumia watu tofauti badala yake zitumie kwa wahusika walioorodheshwa katika bima hiyo tu Jambo ambalo kuwaigiza katika mikono ya sheria na kupata adhabu kali. 2Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF akiwasomea waandishi wa habari maelezo yaliomo katika nyaraka hizo 3Baadhi ya wgonjwa mbalimbali wakisubiri huduma katika hospitali hiyo 4Baadhi ya wgonjwa mbalimbali wakipata huduma katika hospitali hiyo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*