Na Francis Godwin Blog CHUO
cha ufundi stadi (VETA ) nyanda za juu kusini imetangaza vyuo 30
vilivyosajiliwa na vyenye sifa ya kutoa elimu ya mafunzo mbali mbali
yakiwemo ya Hoteli na utalii mkoa wa Iringa na kuwataka wazazi
kutopeleka watoto wao katika vyuo visivyosajiliwa na VETA.
Akitangaza
vyuo hivyo vyenye sifa ya kuendelea kutoa mafunzo mbali mbali
leo mbele ya wanahabari na wamiliki wa vyuo hivyo vilivyosajiliwa
mkoani hapa jana kaimu mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini Bi
Suzana Magani alisema kuwa lengo la kuvitangaza vyuo hivyo ni
kutaka kuepusha utapeli ambao wazazi na wanafunzi wamekuwa
wakikutana nao kutoka katika baadhi ya vyuo ambavyo havitambuliwi na
VETA.
Hivyo
alisema kuwa kuanzia sasa ni vema wazazi kuepuka kupeleka watoto
wao katika vyuo ambavyo havitambuliki na VETA kwani kufanya hivyo
ni sawa na kupoteza fedha na muda wa mtoto kuwepo katika chuo
kisichotambulika.
"
VETA ilifuta
usajili wa usajili wa vyuo vyote mwaka 2009 na mwaka 2010 ilifanya
ukaguzi kwa vyuo vyote na mwaka huu 2014 imeanza kutoa vyeti vya
usajili kwa vyuo ambavyo vinasifa ya kuitwa vyuo vya ufundi na
vyuo vya kutoa mafunzo ya hoteli na utalii katika mikoa yote nchini na
katika mkoa wa Iringa hadi leo Septemba 12 ni vyuo 30 pekee ndivyo
vyenye sifa ya kuitwa vyuo" alisema mkurugenzi huyo
Kuwa
kwa muda wote
huo baada ya vyuo hivyo kufutiwa usajili VETA kilikuwa na jukumu
la kutoa mafunzo mbali mbali ya uboreshaji wa vyuo kwa wamiliki wa
vyuo hivyo na hadi sasa wamiliki wa vyuo 30 pekee ndio
wamefanikiwa kuviwezesha vyuo vyao kuwa na sifa ya kuitwa chuo .
"
Hivyo wito wangu kwa wamiliki wote wa vyuo ambavyo leo mmepata
usajili wa kudumu na VETA jambo ambalo mnapaswa kufanya kuanza
kuvitangaza vyuo vyenu
katika vyombo mbali mbali vya habari ili kuwanusuru wazazi na
wanafunzi wanaoendelea kurubuniwa na vyuo visivyo na sifa na
havitambuliwi na VETA"
Alisema
kuwa kuvitangaza vyuo hivyo na fani zinazotolewa kutasaidia wazazi
kuchagua chuo cha kumpeleka mtoto kupata elimu na kuwa usajili
huo kwa chuo unapaswa kuwa ni usajili endelevu na sio chuo toka
kimesajiliwa hakina kozi mpya zaidi ya kuendelea na kozi za
zamani na madaraja yale yale "
Hivyo alisema usajili huo unapaswa kuwa endelevu kwa kubuni kozi mpya kulingana na miaka inavyosonga mbele .
Bi
Mgani aliwataka wamiliki wa vyuo ambavyo havijasajiliwa kufika
kusajili vyuo vyao kabla ya ofisi yake kuanza msako wa kuvifungia
vyuo hivyo kama ilivyofanyika katika mkoa wa Ruvuma na Njombe .
Alivitaja
vyuo bora 30 ambavyo vimesajiliwa katika mkoa wa Iringa na
kuwataka wazazi kuepuka na vyuo bubu ambavyo havitambuliki na VETA
kuwa ni pamoja na Mufindi VTC, Ifunda Technical Secondary School ,
Mgongo Catholic VTC,
Amani VTC, Mafinga Secretarial College, Nyabula VTC, KIlolo VTC,
Isimani VTC, Sanaa House VTC, Matumaini Centre VTC, Incoment VTC,
Mafinga Lutherani VTC, Kibidula Agriculture VTC, na Ifunda Mission VTC
Vingine
ni Cory Training College, Ilula Institute of Technology and Business
Studies , Starcom Hotel Academy ,Ruaha Tourism College , Southern
College of Tanzania , Tabez VTC, Ng'ingula VTC, ST. Jerome VTC, Ulete
VTC, Upendo VTC, ST. Therese VTC,ST Maria Goreett VTC, SCim Brothers
VTC, Nyota ya asubuhi VTC na Don Bosco Youth Trainging
Centre
Kwa
upande wake mratibu VETA nyanda za juu kusini Bw John Mwanja
alisema kuwa wazazi wasidanganyike na utapeli unaofanywa na baadhi
ya wamiliki wa vyuo kwa kutangaza kuwa wanatoa Dimploma na kuwa
katika mkoa wa Iringa zaidi ya vyuo vikuu kama cha Iringa na Ruaha
na kile cha Iringa RETCO Bussiness hakuna chuo chenye sifa ya kutoa
Diploma ndani ya mkoa wa Iringa .
Hata
hivyo alisema kuwa hakuna chuo kinachosajiliwa NECTA bila ya VETA
kujua na kuwa vyuo vinavyodai vimesajiliwa na NECTA ni utapeli wa
hali ya juu kwani hadi sasa VETA imewasiliana na NECTA makao makuu
hawavitambui vyuo hivyo na kuwa kuendeelea kutoa elimu bila
kusajiliwa ni wizi na mmiliki anapaswa kuwajibishwa kisheria na wao
kama VETA baada ya kuhitimisha zoezi hilo watatoa ripoti katika
vyombo husika vya kisheria ili kuchukua
hatua juu ya vyuo hivyo.
Alisema
baadhi ya vyuo hivyo feki vimekuwa vikitoa elimu ya chuo bila ya
kuwa na mtaala wa VETA na wengi wanatumia uzoefu wao walioupata na
sio sifa za zinazotambuliwa na VETA.
Mkuu
wa chuo cha Mufindi VTC Bw Fredy Kigola mbali ya kuipongeza VETA
kwa mafunzo mbali mbali wanayoyatoa bado alisema kuwa ubora wa
elimu hauwezi kufanikiwa iwapo watoto watafundishwa katika vyuo feki
na kudai kuwa chuo chake kimeendelea kupata umaarufu mkubwa kwa
wazazi kutoka nje na ndani ya Mufindi kupeleka watoto katika chuo
hicho kutoka na ubora wa mafunzo yanayotolewa baada ya VETA kuwapa
elimu ya ziada.
Kigola
alisema kuwa uamuzi wa VETA wa kuvifunga vyuo bubu utasaidia
kuboresha mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo .
Wakati mkuu wa chuo cha cha Utalii Ruaha Bw Yohanes Sanga akitaka wakuu wa vyuo vilivyosajiliwa
mkoani Iringa kuungana kwa kuanzisha chama chao ili kinapoibuka chuo kisichosajiliwa kuweza kupaza sauti ya pamoja.
|
Comments