Walawala CUP kuwasha moto Muheza

Mratibu wa mashindano ya OG Walawala Cup,Omari George (kulia) akipokea jezi zitakazotumika katika mashindano hayo kutoka Meneja Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abas Ali Isere katika hafla fupi iliyofanyika Dar es Salaam jana.



Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya kuwania Kombe la Walawala wilayani Muheza linatarajia kuanza mapema mwezi huu katika uwanja wa Jitegemee.

Mratibu wa Mashindano hayo, Omari George (OG)akizungumza mjini Dar es Salaam jana alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika ambayo ni pamoja na kuandaa vifaa vya michezo.

Alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yamelenga kuibua vipaji vya wachezaji watakaochukua nafasi ya wachezaji waliowahi kuwika zamani na kujenga heshima ya wilaya Muheza kama vile Kasongo Athumani, ISsa Athumani Mgaya na James Kisaka.

OG alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kutoka mwaka 2010 kila timu shiriki hupatiwa jezi na washindi hupata zawadi mbalimbali kama vile vikombe, mipira na sare za michezo.

Alisema katika mashindano ya mwaka huu kila timu imepewa jezi seti moja, sare  kwa ajili ya makocha wa timu 18 zinazoshiriki mashindano hayo, sare kwa viongozi wa Chama cha Soka Wilayani (TFF) na waamuzi watakaochezesha mashindano hayo.


Mratibu huyo alisema amekuwa akishirikiana na Kampuni ya Isere kuandaa vifaa vinabyotumika katika mashindano hayo Kutoka mashindano ya Walawala Cup yaanzishwe timu zilizowahi kutwaa ubingwa ni Polisi (2011), City Boys (2012) na Bambino (2013)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI