Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe leo amezindua magari 54 ya abiria
ya Chama cha Ushirika cha Madereva wa Taksi katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam yenye thamani
ya sh. Milioni 840 kuboresha usafiri wa abiria.Hafla
hiyo ya uzinduzi imefanyika katika eneo la kiwanja cha zamani cha
Ndege, Terminal I, makao makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA) ambapo ameiagiza TAA kuhakikisha inaipa hadhi JNIA kama alivyokuwa
mwenye jina hilo, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.“TAA
hakikisheni JNIA inabeba jina la Julius Nyerere kwa mandhari, utendaji
na vyombo vya usafiri, “ Waziri Mwakyembe amemweleza Mkurugenzi wa JNIA,
Bw. Moses Malaki na uongozi wa TAA kwa jumla.Waziri
Mwakyembe amesema, hatua ya ATACOS kununua magari hayo inaongeza ubora
wa huduma na hadhi ya kiwanja cha ndege cha JNIA na kwamba magari hayo
yatasaidia kuchukua hata wageni wa Serikali
Alisema
mradi huo wa magari ni mkubwa kwa wana ushirika hao na magari yao ni ya
viwango vya juu na hata kwa mbali ukiyaangalia magari hayo, yana
viwango vikubwa na Serikali ikipata wageni zaidi ya 500 kwa mpigo,
haitahangika kutafuta magari kwani hayo yapo. Thamani ya gari moja ni
sh. Milioni 15 na ni mkopo wa Equity Bank.
Hata
hivyo, Waziri Mwakyembe amewataka madereva hao kuzingatia usafi wa
magari na wao wenyewe kwani wageni wakikodi magari hayo na kuyakuta ni
nadhifu na wao ni wasafi, ndio kielelezo cha nchi yetu.
“Naheshimu
sana kazi mnayofanya. Ina add value (ongeza thamani), “ waziri
Mwakyembe amesema na kuutaka uongozi wa TAA utambue mchango wa madereva
hao kwani magari yao ni mazuri na hata katika jengo la tatu la abiria
(TB III) linalojengwa, yanaweza kupewa fursa.
Amewataka
kuyatunza kwa kuyavika vita vyeupe na wao kuvaa sare nyeupe na
kusimamia viwango kwa kuwa na zaidi ya sare moja nyeupe ili hata
akiingia mtalii, ajue kuwa anaingia nchi ya wastarabu.
Hata
hivyo, Waziri Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na madereva hao
kuushitaki uongozi wa TAA mahakamani kuhusu haki ya kuendesha biashara
ya taksi JNIA. Amewaeleza asingeweza kuwasaidia kutatua kero hiyo kwa
kuwa kuna kesi hiyo bado iko mahakamani hadi leo.
“Sijui
nani aliwashauri. Mimi ni Kiongozi wa Serikali tena ni Wakili wa
Mahakama Kuu. Siwezi kuingilia utendaji wa mhimili mwingine wa chombo
cha haki. Nitaonekana wa ajabu. Mikono yangu imefungwa katika hili, “
aliwaeleza na kuacha kujibu kero zao kuhusu mgogoro huo.
Katika
risala yao kwa Waziri Mwakyembe, Katibu wa stendi ya madereva teksi
JNIA, Mohammed Mashombo amemweleza Waziri mafanikio na kero zao tangu
waanze 2000 na kuomba awasaidie.
Hata
hivyo, uongozi wa TAA ulimweleza Waziri Mwakyembe awali kuwa, madereva
hao waliushitaki kuhusiana na mkataba wa kufanya biashara JNIA na kesi
hiyo inaendelea hadi leo na kwamba mengi ya madai waliyomtaka awasaidie,
ndio wameyewasilisha mahakamani.
Hafla
hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali na watendaji wa TAA, Kamanda wa
Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Meneja
wa TRA Mkoa wa Temeke, Mkurugenzi wa Equity Bank, Mkurugenzi wa ABG na
Afisa Biashara wa Manispaa Temeke.
Imetolewa na Godfrey John Lutego
Afisa Uhusiano – Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
Comments