ZIARA YA KINANA HANDENI,TANGA

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiimba kwa hisia wimbo wa uliotungwa enzi hizo na babake Moses Mnauye katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Soko la zamani mjini Handeni wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010/2015 iliyoanza mkoani Tanga baada ya kumaliza ziara ya siku 9 katika mkoa wa Pwani
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mbunge wa Jimbo la Handeni ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi yaCCM katika jimbo hilo.
Waendehsa bodaboda na wananchi wengine wakiwa wamemzingira Kinana kutoa malalamiko yao hasa wanavyonyanyanyaswa na polisi wakaiwa katika shughuli zao mjini Handeni, Tanga.
Kinana akilakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu alipowasli katika Kata ya Mkata wilayani humo, kuanza ziara ya siku 11 katika Mkoa wa Tanga.
Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi baada ya kumaliza ziara ya Mkoa wa Pwani na kuanza ziara ya Mkoa wa Tanga.
Kinana akikumbatiana kwa furaha na Mbunge wa Jimbo la Handeni, Dk. Abdallah Kigoda alipowasili katika Kata ya Mkata kuzindua mradi wa maji wenye zaidi ya sh. bil 2.
Kinana akisalimiana na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa wakati wa mapokezi katika Kata ya Mkata wilayani Handeni.
Kinana akivishwa skafu wakati wa mapokezi hayo
Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma ya selo ya kabila la wazigua wakati wa mapokezi hayo.
Kinana akiangalia ngoma hiyo ya selo
Kinana akikagua mabomba ya mradi huo maji
Kinana na Kigoda wakisaidia kubeba mabomba yaliyokuwa yakishushwa kutoka kwenye lori
Kinana akiweka zege eneo litakapowekwa tanki ikiwa ni ishara ya uzinduazi wa mradi huo
Mbunge wa Jimbo la Handeni, Kigoda akishindilia zege eneo hilo la kuweka tangi katika mradi huo.
Kinana akiangalia ngoma alipowasili katika Kijiji cha Kwalugulu kushiriki katika ujenzi wa majengo ya maabara katika Shule ya Sekondari ya Kwalugulu wilayani Handeni
Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari ya Kwalugulu wilayani Handeni Tanga.
Kinana akisalimiana na baadhi ya wazee alipowasili katika Kijiji cha Kwenjugo kushiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Kwenjugo wilayani Handeni.
Huyu ndiyo Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu akitabasamu alipokuwa akisikiliza hotuba ya Kinana katika Kijiji cha Kwenjugo wilayani humo.
Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kwenjugo wilayani Handeni
Kinana akihutubia mkutano wa hadhara mjini Handeni
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu akielezea kuhusu miradi iliyotekelezwa na inayotekelezwa wilayani humo kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya CCM
Msafara ukiondoka kwenye viwanja vya Soko la zamani mjini Handeni baada mkutano kumalizika

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.