Airtel yazindua Mashindano ya kuvumbua vipaji vya Muziki



  Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star" kwa lengo la kukuza  na kuvumbua vipaji vya wana muziki chipukizi na kuwawezesha
kufikia ndoto zao.  Program hii ni kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon, uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam.
 Mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimples  akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star"kwa lengo la kukuza  na kuvumbua vipaji vya wana muziki chipukizi na kuwawezesha kufikia ndoto zao.  Program hii ni kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon. uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam
 Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi Kipya AY na Mtangazaji maarufu nchini Salam Jabiri wakiwa na baadhi ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo " Airtel TRACE Music Star Program inayoendeshwa
ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon. uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam
 baadhi ya waandishi wa habari na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Airtel Trace Music Star
 Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiwa na msaani wa muziki wa kizazi kipya Lady JD wakati wa uzinduzi wa Airtel Trace Music Star
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akifatilia kwa karibu uzinduzi wa program ya kusaka vipaji vya muziki ijulikanayo kama Airtel Trace Music Star.

Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akiongea wakati wa Uzinduzi wa program ya Airtel Trace Music Star , program itakayowawezesha wanamuziki chipukizi kuonyesha vipaji vyao vya muziki kwa kupitia simu zao za mkononi.

======  ======  =======
Airtel yazindua Mashindano ya kuvumbua vipaji vya Muziki
·        Wanamuziki chipukizi kutoka nchi 13 Afrika kupata nafasi ya
kuonesha uwezo wa wa kuimba na kushinda zawadi kabambe

·       Program hii ni kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya
Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mashindano ya
kusaka vipaji vya muziki kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama
Airtel TRACE Music Star kwa lengo la kukuza vipaji vya muziki na
kuwawezesha wanamuziki chipukizi wa kitanzania kujulikana katika anga
za muziki duniani

Uzinduzi huu umefatia ushirikiano kati ya Airtel na Kampuni Muziki ya
TRACE pamoja na mwanamuziki nguli wa Marekani Akon

Mashindano haya mbali na kufanyika nchini Tanzania pia yatashirikisha
vijana kutoka nchi 13 barani Afrika ambazo Airtel inafanya biashara
zake, nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi,
Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic
Republic of Congo (DRC), na Gabon, ambapo waimbaji bora kutoka kwenye
kila nchi watachaguliwa na kuzawadiwa baada ya kuingizwa kwenye
mashindano yatakayowashirikisha waimbaji bora kutoka nchi nyingine ili
kupata mshindi atakayetwaa taji la Mwanamuziki mwenye kipaji bora
Afrika.  Mshindi wa Afrika atajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo
kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni
pamoja na kufaidika na mafunzo ya kufuliwa kimuziki na Nguli wa Muziki
wa Amerika Akon

Akiongea wakati wa uzinduzi wa program hiyo Mkurugenzi wa Masoko bwana Levi Nyakundi alisema” mpango huu unaenda sambamba na dhamira yetu wa kuwawezesha vijana wenye ndoto ya kuwa wanamuziki bora kuonyesha uwezo wao kuwawezesha kufikia ndoto zao. 

Tunafahamu kuwa Tanzania ina vijana
wengi wenye vipaji vya muziki lakini bado hawajajulikana katika anga
za muziki na ndio maana leo tunazindua program hii na kuwawezesha
kujiunga kirahisi kupitia simu yake ya mkononi na kushirikia Airtel
Trace Music Stars na kuibuka kuwa wanamziki bora”

Mashindano haya yatakayoenda kwa muda wa mienzi sita yanaanza kuanzia rasmi hapa nchini siku octoba 7 2014 ambapo mshiriki yeyote
atakayependa kushiriki atatakiwa kupiga 0901002233, na kuimba nyimbo
zake kwa kutumia simu yake na kutuma kwenye namba hii, kisha nyimbo
zake zitasikilizwa na kuchagulia kufudhu kuingia kwenye kinyanganyiro
na kuweza kupigiwa kura kuibuka kuwa mwimbaji nyota wa Tanzania na
baadae kuwa super star wa Afrika kwa ujumla

Halikadhalika mashabiki na wapenzi wa muziki wataweza kumpigia kura
mshiriki wanayempenda ili kumuwezeshwa nyimbo zake kushinda, ili
kumpigia kura mshiriki wako tuma namba/code ambayo mshiriki
ataitangaza pindi nyimbo yake itakapochaguliwa kuingia kwenye
mashindano au unaweza kuipata wewe mwenyewe kwenye tovuti
www.tracemusicstar.com’’
Aliongeza Nyakundi
Akiongea kuhusu program hiyo Mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimples,alisema’ kwa hakika haya ni mashindano ya pekee yanayotoa fulsa kwa mwanamziki yeyote ambaye angependa kuwa superstar kushiriki.

Napenda kuwahamasisha vijana kuchangamkia fulsa hii kwa kurekodi
freestyle yako ya  flave yoyote kali  kupitia simu yako na kutuma
nyimbo yako. Pia napenda kuwaomba mashabiki na wapenzi wa muziki
kuwapigia kura washiriki hawa kwa wingi ili kuweza kumpata ushindi.
kwa wanamuziki chipukizi mashindano haya si yakukosa maana wewe pia
unaweza kuibuka kuwa superstar wa Airtel Trace Music Star kwa njia
rahisi tu Piga, Imba, Shinda. aliongeza Dimples

Airtel imeingia mkataba wa ushirikiano na Trace Music kwa  muda wa
miaka mitatu ambapo Fainali ya mashindano haya ya Airtel Trace Music
2014 yanategemea kufanyika Mwezi March 2015.

Zawadi nyingine zitakazotoliwa kwa washindi wa mashindano haya ni
pamoja na pesa taslimu na simu za mkononi

Kwa maelezo zaid tembelea tovuti ya:  www.tracemusicstar.com /
Facebook: https://www.facebook.com/airteltracemusicstar
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA