IBADA MAALUM YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU DR. WILLIAM SHIJA KABLA YA KURUDISHWA TANZANIA



Mke wa Marehemu, Mama Getrude Shija (kushoto), akifuatana na Mama Balozi (Joyce Kallaghe), ndugu, jamaa na marafiki, wakiingia kanisani kushiriki Ibada maalum ya kuuaga Mwili wa Marehemu Dk. William Shija.

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Commonwealth Parliamentary Association (CPA), Dr. William Shija, aliyefariki dunia Jumamosi ya Tarehe 4 Oktoba 2014, umeagwa rasmi jana katika Ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Vincent de Paulo, Osterley, London.

Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe na maafisa wa Ubalozi, ndugu, jamaa na marafiki na wafanyakazi wengine wa ubalozi walikuwepo Kanisani hapo. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwa Shirika la ndege la Emirates kwenda Dar es salaam, na hatimaye Sengerema kwa mazishi.

Mungu aiweke roho ya Marehemu Dk. William Shija mahala pema Peponi ( Amin)
Mwili wa Marehemu Dk. William Shija ukiingizwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Vincent de Paulo kwa Ibada maalum na kuagwa rasmi na ndugu na jamaa wa marehemu.
Father Mark wa Kanisa Katoliki la Vicent de Paulo, akiongoza Ibada maalum ya kuuga mwili wa marehemu Dk. William Shija Kanisani hapo.
Mama Balozi Joyce Kallaghe(kushoto), Mke wa Marehemu, mama Getrude Shija, Watoto wa Marehemu, Ndugu na jamaa wa marehemu wakiwa kwenye Ibada ya kuuga Mwili wa Marehemu.
Mama Balozi Joyce Kallaghe(kushoto), Mke wa Marehemu, mama Getrude Shija, watoto wa Marehemu, Ndugu na jamaa wa marehemu wakiwa kwenye Ibada ya kuuga Mwili wa Marehemu
Monica William Shija, mtoto wa Marehemu, akiongoza somo moja katika Ibada hiyo maalum ya kuuga Mwili wa Marehemu Dk. William Shija.

Father Mark akimpa mkono wa pole Mke wa Marehemu, mama Gertude mara baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo maalum iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Vincent de Paulo.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe akipeana mkono na Father Mark mara baada ya kumalizika kwa Ibada maalum ya kuuga Mwili wa Marehemu Dk. William Shija.
Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe, akijumuika pamoja na familia ya marehemu Dk. William Shija, Ndugu, Jamaa na marafiki waliofika Kanisani hapo kuuaga mwili wa marehemu kwenye Ibada maalum iliyoandaliwa kwenye kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Vicent de Paulo, London.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*