KINANA ANYWA CHAI NYUMBANI KWA BALOZI WA SHINA, MSOSI WA MCHANA KWA MAMA LISHE IRINGA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata mlo nyumbani kwa Balozi Lucas Mtumbuka (kushoto)wa Shina namba moja eneo la Mkimbizi, alipokwenda kumtembelea yeye na wananchama wake wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Jimbo la Iringa Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akichukua mhogo ambao ni sehemu ya vyakula alivyoandaliwa na balozi
 Watoto wakipanda kwenye uzio wa nyumba ili wapate kumuona Kinana alipomtembelea Balozi, Lucas Mtumbuka, eneo la Mkimbizi
 Kinana akiingia kwenye ukumbi kuzungumza na wanachama 707 wa kikundi cha Iringa Masoko Vicoba ambapo aliahidi kuwasaidia kuipata mkopo mkubwa wa fedha watakazokuwa wanakopeshana.
 Kinana akizungumza na madereva wa daladala baada ya kuzindua tawi la wakareketwa wa CCM, mjini Iringa leo. Tawi hilo lina wanachama 60.
 Mama Lishe akimnawisha mikono Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambapo yeye na viongozi pamoja na baadhi ya wananchama wa CCM walikwenda kupata chakula cha mchana kwa mama lishe katika Soko Kuu la Iringa leo.
 Kinana akiapata mlo wa mchana kwa mama lishe mjini Iringa  leo wakati wa mapumziko ya ziara ya kuimarisha uhai wa chama.Kulia ni Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya Iringa Mjini, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu.
 Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati (kushoto) akiwa na viongozi wengine wa CCM wakipata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, mjini Iringa leo.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga (katikati) akiwa na viongozi wengine wa CCM wakati wa chakula cha mchana kwa mama lishe.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chongolo, akipata mlo huo wa mchana kwa mama lishe.
 Wanahabari ambao baadhi yao wako kwenye msafara wa Kinana  wakipata mlo wa mchana kwa mama lishe
Kinana akiondoka baada ya kupata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, katika Soko la Iringa Mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA