Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Ikulu wakiwavuta timu ya Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula (hawapo pichani) wakati wa mashindano ya kuingia hatua ya nusu fainali mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro ambapo Ikulu imefuzu kucheza hatua hiyo.Timu ya kuvuta kamba ya wanaume ya Ikulu wakiwavuta timu ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA- hawapo pichani) wakati wa mashindano ya kuingia hatua ya nusu fainali mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro ambapo Ikulu imefuzu kucheza hatua hiyo.Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao wa kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa goli 1- 0 leo mjini Morogoro.
Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia) wakiomba dua kabla ya mchezo wa hatua ya robo fainali leo mjini Morogoro.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (waliovalia sare ya bluu) wakisalimiana na wachezaji wa mchezo huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (waliovalia sare ya rangi ya machungwa) kabla ya mchezo wa robo fainali ambapo timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wameibuka washindi na kuingia nusu fainali katika mshindano ya SHIMIWI kwa kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu 1- 0 Mchezaji wa timu ya mpira wa pete Ikulu Mwadawa Twalibu (GA) akimiliki mpira wakati wa mchezo wa robo fainali kati ya timu ya Ikulu na Bunge wa kumsaka mshindi atakayecheza nusu fainali, timu ya Ikulu imefuzu kwa kuwashinda timu ya Bunge kwa magoli 67 kwa 24.
Baadhi ya watumishi wanaoshabikia mchezo wa drafti wakishuhudia pambano la kuwatafuta washindi wa mcheo huo leo katika kiwanja cha Jamhuri mjini Morogoro.
Mshindi wa kwanza wa mchezo wa drafti wanaume Salumu Simba (kushoto) kutoka RAS Dodoma akichuana na mshindi wa tatu wa mchezo huo Ramadhani Mtenga (kulia)kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro.
……………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati siku ya Jumamosi Oktoba 11 mwaka huu na kuhusisha fainali za michezo mbalimbali ambazo zitachezwa kuhitimisha mashindano hayo ambapo yatafungwa rasmi kwa maandamano ya wanamichezo yatakayopokewa na Mgeni Rasmi atakayefunga michezo hiyo.
Comments