MBUNGE KIGOLA AGEUKWA NA WAPIGA KURA MBELE YA WAZIRI NYALANDU

Kigola akifurahi kabla kibao hakijageukNasifiwe Ponziano Miwoo mbele ya Waziri Nyalandu alipokuwa akihoji uadilifu wa mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola


SAKATA la  vibali vya uvunaji miti katika msitu wa Taifa wa Sao Hill
Mufindi mkoani Iringa limemuweka pabaya mbunge wa  jimbo la Mufindi
kusini Mendrad Kigola baada ya wapiga kura  wake kumgeuka mbele ya
waziri maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  kuwa mbunge huyo ni
mchochezi katika  sakata  hilo.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Igowole juzi
Kigola alimkaribisha waziri huyo huku akikosoa mgao wa vibali vya
kuvuna miti katika msitu wa Taifa wa saohill ambao sehemu yake upo
katika jimbo hilo, ulivyofanywa kwa vikundi vya wajasiriamali wa
wilaya ya Mufindi.

Huku akipigiwa makofi ya mara kwa mara yaliyomfanya ashindwe kusimama
sehemu moja wakati akiongea, Kigola alisema: “sina pingamizi dhidi ya
watu na vijiji vilivyopata mgao wa mwaka huu.”

“Shida yangu ni mgao uliotolewa kwa vikundi vya wilaya ya Mufindi
yenye majimbo mawili. Wakati jimbo langu la Mufindi Kusini vimepata
vikundi 12 kati ya 48, vingine vyote vilivyobaki vimetoka upande
mwingine. Mheshimiwa waziri, nakuomba ulione hilo,” alisema.

Kauli ya Kigola ilitafsiriwa na baadhi ya watu waliokuwepo katika
mkutano huo kwamba ilikuwa ikimpiga vijembe mbunge wa jimbo jirani la
Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii.

Taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya
ya Mufindi zinadai kwamba Mgimwa na Kigola hawapikiki chungu kimoja
ikiwa ni matokeo ya kinachoelezwa na walio jirani na wabunge hao
kwamba mmoja wao ana wivu wa kisiasa dhidi ya mwenzake.

Taarifa hizo zisizo rasmi ambazo hata hivyo hazijawahi kutolewa
ufafanuzi na Kigola mwenyewe zinadai kwamba amekuwa akimuonea wivu
Mgimwa baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri.

Wivu huo ndio umepelekea kuchochea chokochoko ya kuhoji uwiano wa mgao
wa vibali vikiwemo vibali 48 vilivyotolewa kwa vikundi 48 vya wilaya
ya Mufindi.

Hoja ya Kigola dhidi ya mgao wa vibali hivyo ilionekana ina mashiko
kwa muda wote wa mkutano huo mpaka pale Waziri Nyalandu alipotoa ruksa
kwa wananchi wa kijiji hicho cha Igowole kuuliza maswali.


Alikuwa Nasifiwe Ponziano Miwoo aliyechafua hali ya hewamara baada ya
kupata nafasi ya kuuliza swali alilotoa kwa mtindo aliodai wa kujenga
hoja ili wananchi wamuelewe.

Akinukuu vifungu kadhaa vya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano huku
akioanisha na uadilifu wa mbunge huyo Miwoo alisema:

“Kuna haja ya kuoanisha hoja za mbunge huyu Kigola na uadilifu wake;
na kuna haja ya kujua mali zinazomilikiwa na mbunge huyu ili tuone
kama kunasababu kwa familia yake kupata kibali cha kuvuna miti wakati
baadhi ya vijiji na vya wilaya ya Mufindi na wajasiriamali wake
wakikosa,” alisema.

Alisema katika orodha ya wanufaika na vibali vya mwaka huu, jina namba
388 ni la mtoto wa Kigola anayesoma katika moja ya shule bora zilizoko
wilayani Mufindi.
Alisema zipo dalili kwamba Kigola alitumia jina la mwanae huyo kupata
kibali hicho jambo linalojenga mashaka dhidi ya uadilifu wake.

“Mheshimiwa Waziri tuna mashaka na huyu mtu na kama kila mwaka anajaza
fomu inayoonesha mali anazomilikia. Kwanini jina la mwanae litumike,”
Miwoo alisema huku waliokuwa wakimshangilia Kigola wakigeuza kibao na
kumshangilia yeye.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*