Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika waendelea – Benki ya Dunia

      


??????????Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa nyuma yake ni Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya DSCI0059Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
??????????Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
??????????Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
…………………………………………………………
Na Ingiahedi Mduma-Washington D.C
Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika hufanyika kila mwaka wakati wa mikutani ya Benki ya Dunia na IMF na unahusisha kundi la nchi za Benki ya Dunia ambazo zinapata mikopo nafuu kutoka IDA. IDA ni shirika au mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia.
Katika mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za kibenki na mambo ya utawala kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa mikutano hiyo na kamati mbalimbali. Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri wa Fedha. Kwa mwaka 2014 -16 Mwenyekiti atakuwa Waziri wa Fedha kutoka Ethiopia na Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi hawa wataongoza mpaka mwaka 2016. Mwaziri wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni MaGavana mbadala, hivi ni vyeo vya uwakilishi kattika Benki ya Dunia.
Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake alisema kuwa”tumepata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza la nchi za Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake anatoka Zimbabwe “ alisema.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa anayemaliza muda wake anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa kura na kila nchi. “Hawa watakuwa watendaji moja kwa moja kuanzia sasa na nafasi hizi zinapatikana kwa mzunguko.”alisisitiza..
Vilevile katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo ambayo itakuwa na mwenyekiti ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka Tanzania, Namibia pamoja na Sierralion.
Jambo lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni kwamba Benki itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea toka kwenye mfuko wa IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika.
Vilevile walisisistiza suala la gonjwa la EBOLA. Walielezea kuwa wataendelea kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo tatizo.
Pia Benki ya Dunia itaendelea kupeleka wafanyakazi kujifunza jinsi Benki ya Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu kuchagua watu wazuri ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze kutumia ujuzi wanao upata.
Mwisho walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia jitihada ambazo zinalenga matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya kazi kwa kuzingatia matwakwa ya BRN. Hivyo wanatagemea fedha zinazotolewa zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa sasa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI