Mtangazaji mahiri wa RTD Ben Kiko afariki dunia

Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko enzi za uhai wake akiwa katika moja ya semina alizohudhuria.

MTANGAZAJI na mwandishi wa habari mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Ben Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.

MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA,
AMIN
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kikoakizungumza na Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini Dixon Busagaga alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Cheyo mkoani Tabora wakati wa uhai wake.



Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo (pichani akiwa ameshika hati ya Tuzo ya Utumishi uliotukuka wa Maisha April 2012) maarufu kama Ben Kiko,   
 atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*