OFISI YA MASIJALA YA IDARA YA ARDHI YACHOMWA MOTO KIGOMA




Watu wanne wanashikiliwa na polisi mkoani Kigoma kwa tuhuma za kuchoma moto ofisi ya masijala ya Idara ya Ardhi ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuteketeza hati na nyaraka mbalimbali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Ibrahim, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Anna Fanuel (46), Makrina Paul (49), Saimon Pius (37) na Tumaini Esau (44).
Alisema Oktoba mosi, mwaka huu saa 4.15 usiku, ofisi ya masijala ya idara hiyo ilichomwa moto na kuteketeza hati na nyaraka mbalimbali. Kamanda Ibrahim alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kitendo hicho ni njama za kupoteza vielelezo nyeti.

Alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa idara hiyo imegubikwa na migogoro inayohusiana na ugawaji wa viwanja.

“Uchunguzi wetu wa awali unaonyesha watu hao walitumia mafuta ya petroli kuchoma ofisi hiyo…tunaendelea kufuatilia zaidi tukio hili,” alisema Ibrahim.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.