STARTIMES YAFUNGUA DUKA JIPYA MTAA WA SAMORA JIJINI DAR ES SALAAM



 Nembo ya Startimes inavyoonekana.
 Duka hilo linavyoonekana kwa nje.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Startimes Tanzania, Lanfang Liao akizungumza na wanahari wakati wa ufunguzi wa duka hilo.
 Mkurugenzi wa Oparesheni  wa Kampuni hiyo, Geng Jlan Xun, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Startimes Tanzania, Lanfang Liao (katikati), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka hilo. Wanashuhudia kulia ni  Mkurugenzi wa Oparesheni  wa Kampuni hiyo, Geng Jlan Xun na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Zuhura Hanif. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
 Wafanyakazi wa duka hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
  Mkurugenzi wa Oparesheni  wa Kampuni hiyo, Geng Jlan Xun (kushoto), akihojiwa na wanahabari.
 Mpiga picha wa Kituo cha Channel Ten, Bi. Faudhia akichukua tukio hilo.
Wafanyakazi wa duka hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja.


Dotto Mwaibale

KAMPUNI  ya Star Times imefungua duka la kutoa huduma kwa wateja ikiwa ni njia ya moja wapo ya kuboresha upatikanaji wa huduma zake nchini. 

Duka  hilo lipo katika maeneo ya Posta mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.

Akifungua duka hilo Dar es Salaam leo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Startimes Lanfang Liao alisema tokea kuanzishwa kwa maduka ya star times duka hilo ni la sita ambapo maduka mengine yapo Buguruni,Mikocheni-Bamaga,Tegeta,Msimbazi,Ukonga na Samora.

Alisema Star times ina nia ya dhati ya kutoa huduma bora kwa wateja wake ili kuweza kutoa usumbufu unaojitokeza mara kwa mara kwa wateja wao.

"Katika duka hilo kutapatikana kila aina ya huduma kama vile kutengenezewa chaneli,namna ya kuunganishiwa  na ufumbuzi  juu ya matatizo mbalimbali yanayopatikana katika ving'amuzi vyetu,alisema.

Naye,Kaimu Meneja wa duka hilo jipya Saadat Amour alisema wanaendelea kutoa huduma kwa wateja wao ambapo sasa kuna huduma mpya ya nyumba hadi nyumba.

Alisema,katika huduma hiyo ya nyumba hadi nyumba ambapo wateja hutembelewa ili kupatiwa msaada wa ufumbuzi kuhusu huduma zao.

"Wateja wetu walikuwa wanalalamika kwamba kuna tatozo la kugoma kwa chaneli hali hiyo haitakuwepo tena kwani tumeshatengeneza minara miwili mipya,"alisema

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU