WEMA SEPETU ANAKULA MAISHA CHINA

 


WAKATI bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya kuzomewa na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Wema Sepetu ‘Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China, Amani lina full data.Bebi wa mbongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ , Wema Sepetu ‘Madam’. Chanzo makini kilicho ‘kloz’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini, kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha la Fiesta, akiwa
ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake, Martin Kadinda na Petit Man, wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo. Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou nchini humo, Wema na wanaume hao wawili walichukua vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn, inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China. 
“Yaani Wema jamani ana mambo, inavyoonekana lile rhumba la wakati ule ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho inauma. Wewe fikiria mtu amekwenda kuchukua vifaa vya biashara, unakwenda na hao wanaume wa kazi gani kama siyo kupoteza fedha tu,” kilisema chanzo hicho.



Wema Sepetu ‘Madam’ akipozi. Inadaiwa kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi kuliko yoyote duniani, ni ununuzi wa vipodozi, kwani ana mpango wa kufungua duka kubwa katika eneo ambalo halijatajwa jijini Dar es Salaam. 

Baada ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi maisha ya starehe, wakila bata katika klabu mbalimbali za usiku, ambako wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha. 

“Kwa matanuzi anayofanya kule, hata hiyo biashara aliyoifuata haina maana, angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli, angetafuta tu hoteli ya kawaida ili kubana matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa, sasa wewe mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa, tena na wanaume wawili wanakutegemea, hizo pesa si kuzitapanya tu jamani,” kilisema chanzo hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.