AIRTEL YAMWAGA VITABU VYA MILIONI 15 WILAYANI MAKETE -NJOMBE


Meneja wa Kanda za juu kusini wa Airtel bw, Straton Mushi akikabidhi msaada wa vitabu kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete. Anaeshudia kushoto ni mkuu wa shule msaidizi bw, Fadhili Dononda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE na Meneja wa Kanda za juu kusini wa Airtel bw, Straton Mushi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari iwawa wakifurahia baadda ya hafla ya makabidhiano ya msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 15 utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete.

Mradi wa SHULE YETU unaotekelezwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya AIRTEL umeendelea kunufaisha shule kadhaa nchini kwa sasa umeingia wilayani Makete, Mkoani Njombe na kutoa msaada wa Vitabu vya kiada na ziada vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 15 kwa shule tano wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE ndiye aliyepokea shehena ya Vitabu hivyo ambapo pamoja na mambo mengine amesifu Msaada huo kuwa unaunga mkono Juhudi za Rais JAKAYA KIKWETE katika kufanya mabadiliko makubwa katika sayansi na teknolojia nchini kwa kuwekeza kwenye elimu.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo wilayani Makete Mkoani Njombe kwa niaba ya shule zingine zinazofaidika na mradi huo zikiwemo Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.