KINANA AAPA KUWASHUGHULIKIA WALIOHUSIKA KUVIUA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NACHINGWEA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kulima shamba kwa kutumia trekta katika shamba la Umoja Rika katika Kijiji cha Mkotokuyama, wakati wa ziara yake wilayani, Nachingwea, Lindi.ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG



 Kinana akisaidia kung'oa visiki katika shamba la Umoja la Rika baada ya kushiriki kulima kwa kutumia trekta katika Kijiji cha Mkotokuyana, wilayani Nachingwea leo.
 Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akisaidia kung'oa visiki katika shamba la Umoja Rika, Nachingwea leo
 Kinana akizungumza na mmoja wa wananchama waasisi wa TANU, aliyejiunga mwaka 1957, Asha Kanduru (89), alipokuwa akitoka kushiriki kulima shamba kwa trekta katika shamba la Umoja Rika katika Kijiji cha Mkotokuyana, Nachingwea leo.
 Komredi Kinana akiangalia moja ya majiko ya kisasa alipozindua katika Shule ya Sekondari ya Nachingwea
 Wananchi wa Kijiji cha Naipanga aliposhiriki ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Serikalai ya Kijiji hicho, wilayani Nachingwea leo.
 Kinana akisaidia kuweka zege katika rinta ya jengo la Ofisi ya Kijiji cha Naipanga wilayani Nachingwea
 Komredi Kinana akikagua ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Msingi Matangini, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi leo.
 Wapagazi wakishusha magunia ya korosho kutoka kwenye lori kwa ajili ya kuhifadhi kwenye maghala yaliyokuwa kiwanda cha kubangua korosho na kugeuzwa kuwa maghala, kitendo ambacho amekikemea Komred Kinana na kwamba watu wote waliohusika kufanya hivyo wanastahili kushitakiwa. Inadaiwa mkataba wa Serikali wa kuwauzia viwanda wafanyabiashara ilikuwa ni kuviendendeleza si kubadili matumizi.
 Kinana akikagua ghala la kuhifadhia magunia ya korosho, ambalo awali kilikuwa kiwanda cha kubangulia korosho  lakini waliokinunua inadaiwa wameng'oa mitambo na kugeuza kuwa ghala,
 Komredi Kinana akizungumza na baadhi ya madereva wa malori waliokuwa wakilalamikia kitendo cha kucheleweshwa upakuaji wa korosho katika maghala hayo.
 Kinana akikagua kilichokuwa kiwanda cha ufuta ambacho sasa kimegeuzwa ghala la kuhifadhia vifaa vya Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Wilayani Nachingwe, Lindi.
 Wananchi wakishangilia huku wakiwa na picha ya Komredi Kinana alipowasili kwenye Uwanja wa Mashujaa, mjini Nachingwea.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa, mjini Nachingwea leo
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa, mjini Nachingwea ambapo aliwaasa wafuasi wa chama cha CUF, kuachana na chama hicho akidai hakina mwelekeo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mashujaa, mjini Nachingwea, ambapo aliukandia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kuwa umeanza kusambaratika, akidai Chadema wamesambaza waraka unaowahimiza viongozi wao mikoani kuhakikisha kila nafasi ya kugombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Desemba 14, mwaka huu waweke wanawekwa wanachama wa chama hicho tofauti  na makubaliano waliyowekeana na vyama vilivyo kwenye umoja huo.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA