KINANA ALAKIWA KWA SHANGWE MTWARA VIJIJINI, ATOA HESHIMA KWENYE MNARA WA SHUJAA HAMAD MZEE ALIYETUNGUA NDEGE MBILI ZA KIRENO KATIKA VITA VYA UKOMBOZI WA MSUMBIJI

 Wananachi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Mtwara Vijijini, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


 Kinana akizungumza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kibaoni, Mtwara Vijijini leo.
 Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Katika Kijiji cha Nanguruwe, Wilaya Mtwara Vijijini
 Mzee Ismail Lumbeya (95), akisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Nanguruwe
Mnara wa Kumbukumbu ya Mwanajeshi wa Tanzania , Hamad Mzee aliyeuawa na ndege ya kivita ya wareno baada ya kuzitungua ndege mbili za kivita mwaka  1972 katika Kijiji cha Kitaya mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wakati wa mapambano ya kuikomboa Msumbiji

 Kinana akitoa heshima katika mnara wa kumbukumbu shujaa Hamad Mzee katika Kijiji cha Kitaya, Mtwara Vijijini
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Kitaya
 Ngoma ya asili ikitumbuiza wakati wa mkutano huo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo


Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Kinana akipanda katika moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwa makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini katika mkutano wa hadhara wa katika Kata ya Kitaya.
Kinana akimkabidhi kadi ya CCM mmoja wa wanachama wapya wa chama hicho katika mkutano huo
 Watoto wakiwa na vipeperushi vya picha ya Kinana wakati wa mapokezi yake katika Kijiji cha Kibaoni
 Kinana akikunjua bendera wakati wa uzinduzi wa Tawi la CCM la Vijana akatika Kijiji cha Nanyamba
 Kinana akitoka kukagua mradi wa maji katika Kata ya Nanyamba Mtwara Vijijini
 Vijana wakicheza ngoma ya madudu katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Nanyamba

 Kinana akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe kinachotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya Mtwara Vijijini
Kinana akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA