Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu
Michael Chilufya Sata Ikulu mjini Lusaka Zambia jana Novemba 11,2014.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal
wa kwanza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda,
Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza
na Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga
mwili wa Rais Michael Sata iliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye
Uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda
kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa
wakati mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata
yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka
Zambia.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akimfariji Rais mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada
ya kumalizika maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata
kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa
yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akimfariji Rais mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika
mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja
vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana
Novemba 11,2014. katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth
Kaunda.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael
Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi
wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014. (Picha na OMR)
Comments