MSAMA AUCTION MART KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA VIFAA MBALIMBALI VYA KUDURUFU KAZI ZA WASANII

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani), moja kati ya mashine 4 za  kurudufu CD  feki zilizokamatwa katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa wa Polisi, D/SSGT Daniel Gingo.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), wino unaotumika kunakshia makasha ya CD feki wanazozitengeneza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), baadhi ya CD feki zilizokamatwa


=========  =======  =======  =======
KAMPUNI ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama ikishirikiana na Jeshi la Polisi Kituo cha Urafiki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, imekamata kompyuta za kufyatua kazi feki za wasanii zenye thamani ya mil18.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama, alisema mitambo hiyo imekamatwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya pande hizo tatu pamoja na sapoti ya wasamaria wema. Alisema kopyuta, mashine na kazi feki zenye thamani ya mamilioni ya fedha, zimekamatwa eneo la Kimara-Machungwani, jijini Dar es Salaam na mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya mchakato wa kiheria wa kufikishwa mahakamani. 

Msama alisema akiwa mdau wa masuala ya burudani kupitia kampuni yake ya Msama Promotions Ltd ambayo imekuwa ikiratibu matamasha ya Muziki wa Injili, amekuwa akiguswa na kitendo wanjanja wachache kunufaika na jasho la kazi ya wengine.Alisema wizi wa kazi za wasanii mbalimbali umekuwa kikwazo cha mafanikio ya wahusika ambao licha ya kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu, wameshindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana na wajanja hao kuingiza kazi feki mtaani ambazo huuzwa kwa bei ya kutupa.

Msama alisema kazi hiyo ngumu ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni yake kwa kushirikiana na wadau wengine, anashukuru kwamba kadiri siku zinavyosogea wengi wamezidi kukamatwa kutokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakipewa.“Msama Auction Mart tunachukua nafasi hii kulipongeza Jeshi la Polisi hasa Kituo cha Ubungo ambacho wamekuwa msaada mkubwa kwetu katika vita hii ya kupambana na
wezi wa kazi za wasanii,” alisema Msama.

Aliongeza, kwa ushirikiano mkubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, anashukuru kazi hiyo imekuwa ikisonga mbele kwa kazi feki kuzidi kukamatwa katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kulinda maslahi ya wasanii.Alisema tangu kuanza kwa kazi hiyo ngumu ya kukabiliana na wizi wa kazi za wasanii, kampuni yake imekamata vifaa mbalimbali vya kukamilisha kazi hiyo na kazi zenye jumla
ya shilingi bil.12.

Msama alisema kampuni yake imejitwika jukumu hilo zito kwa lengo la kuona wasanii wa Tanzania wananufaika na ubora wa kazi zao katika kuendesha maisha yao kwamba kupitia vipaji vyao, wahusika waweze kujiajiri.Alisema, katika mazingira ya sasa ambapo jasho la wasanii linaishia mikononi mwa wajanja wachache ambao wamekuwa wakichakachua kazi, kamwe wasani hawawezi kupata kipato cha kutosha kuboresha maisha yao.

Msama ametoa wito pia kwa wasamaria wema sio tu kutoa taarifa kwa kampuni yake au Jeshi la Polisi za kuwafichua wanaojihusisha na uchakachuaji wa kazi za wasanii,  pia kuacha kununua kazi feki japo huuzwa kwa bei ya kutupa.Baadhi ya wananchi walioshuhudia baadhi ya vifaa na kazi feki, kwa nyakati tofauti wameipongeza kampuni ya Msama Auction Mart kwa kazi hiyo ngumu kwa maslahi
ya wasanii.

Kelvin Living na Iddy Abbas wa Mabibo, kwa nyakati tofauti, wameomba kazi hiyo iwe endelevu kwa sababu wajanja hao wachache wanachangia wasanii kukosa maslahi mazuri kupitia vipaji vyao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI