PICHA:MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA SHERIA NGOWI AFUNIKA KATIKA MAONYESHO YA MAVAZI YA 'MERCEDES BENZ FASHION WEEK AFRICA 2014' NCHINI AFRIKA KUSINI

Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014001-1 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014002 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014003 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014004 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014005 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014006 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014007 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014008 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014009 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014010 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014011 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014012 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014013 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014014
 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014015
 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014016
 Na Mwandishi wetu 
 Mbunifu wa kimataifa wa mavazi kutoka Tanzania, Sheria Ngowi amedhihirisha kuwa yeye ni nguli katika ubunifu baada ya kufinika katika onyesho la mavazi la kimataifa lijulikanalo kama Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 lililofanyika juzi Ijumaa mjini Johannesburg, Afrika Kusini. 
Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aliyoyaita 'PRIDE' yaani kujivunia, kama moja ya njia za kumuenzi Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere pamoja na viongozi mashuhuri waliopigania uhuru Afrika. Afrika Kusini ilizizima na kuduwaa kwa muda usiopungua dakika 15 pale ambapo mavazi mbali mbali yaliyobuniwa na Ngowi yalipokuwa yakioneshwa katika ukumbi wa Melrose Arch. 
Sheria Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aina ya suti yenye ubunifu na ueledi wa hali ya juu kwa kutumia vitambaa vya kisasa na kale vilivyonakshiwa kwa maua na rangi za kuvutia kama nyekundu, zambarau, machungwa, nyeupe na nyeusi huku mengine yakiwa bila maua lakini yaliyong'aa kwa kutumia rangi imara kama blu, kahawia na kijivu. 
Onyesho hilo la Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 lilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa umma kutoka Afrika kusini, Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Radhia Msuya, wabunifu wa mavazi kutoka nchi za Afrika kama Taibo Bacar kutoka Mozambique, David Tlale kutoka Afrika Kusini, waandishi wa habari kutoka sehemu mbali mbali za dunia na wadau wa mitindo. 
 Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 ni onyesho la kimataifa linalofanyika nchini Afrika Kusini mara moja kwa mwaka likikusanya zaidi ya wabunifu wa mavazi 35 kutoka Afrika kwa ajili ya kuonesha ubunifu wa mavazi yao ambapo kwa mwaka huu Sheria Ngowi ni mbunifu pekee aliyechaguliwa katika onyesho hilo kutoka Tanzania. Sheria Ngowi anasifika kwa ubunifu wa mavazi aina ya suti, kanzu,sare za makampuni, mashirika, shule na hafla mbalimbali kama harusi.
Mbunifu huyu alifungua rasmi ofisi zake zilizopo Masaki, mtaa wa Buzwagi mkabala na Ubalozi wa Angola mwaka mmoja na nusu uliopita ambapo alianza kazi kwa kuwatengenezea mavazi watu kutoka nchi mbalimbali duniani. Pongezi nyingi kwa Sheria Ngowi, unaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kipaji chako na kazi zako nzuri.
 
 
www.Sheriangowi.com

Kwa Habari Zaidi
Twitter:Sheriangowi
Instgram:Sheriangowi
Simu:+255-712 709797

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.