PROFESA MUHONGO ASEMA FEDHA ZILIZOWEKWA KATIKA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW SIO MALI YA UMMA


Profesa, Sospeter Muhongo
Suleiman Msuya

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow na kulipwa Kampuni ya IPTL sio fedha za umma na kutaka watu wanaolishupalia wapuuzwe kwani ni sawa na wapuuzi.

Wakati Waziri Muhongo akiwashutumu wananchi na wabunge ambao wanaonekana kushupalia  suala hilo Serikali kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue amenukuliwa akisema ripoti ya uchunguzi wa suala hilo bado hijakamilika jambo ambalo linaleta mkanganyiko kwa jamii

Muhongo alisema hayo wakati akizungumza na wawekezaji zaidi ya 170 kutoka nchi mbalimbali Duniani jana wakati wa mkutano wa pili wa kujadili jinsi ya kulipatia bara la Afrika umeme kwa siku za karibuni.

Alisema fedha ambazo zilikuwepo katika akaunti hiyo Escrow zilikuwa za IPTL hivyo ni jambo la kusikitisha kuona wanajitokeza watu ambao wanahakikishia kuwa ni za umma.

Peofesa Muhongo alisema iwapo jamii itajikita katika kufikirishwa na watu wachache na kuacha kuangalia uhalisia ni dhahiri kuwa itakuwa inajichelewesha kupiga hatua za kimaendeleo.

"Jamani napenda kusema kujadili suala hili la akaunti ya Tegete Escrow ni sawa na upuuzi kwani fedha hizi sio za umma kama watu wanavyolazimisha iwe (People who are discuss Escrow Account are Ignorant), " alisema maneno hayo Muhongo. 

Suala la akaunti ya Tegete Escrow liliibuliwa Bungeni na Mbunge wa Kasulu Kusini David Kafulila ambaye aliishutumu Serikali kwa kunyamazia upotevu wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 200 sakata ambalo hadi sasa limekuwa likitolewa majibu tofauti na Serikali.

Kutokana na sakata hilo wabunge wengi hasa kutoka vyama vya upinzani wameonyesha kuhitaji ripoti kamili kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) na ili ya Taasisi ya Kuzuia na Kuapambana na Rushwa (PCCB) kuwasilishwa Bungeni jambo ambalo linaendelea kuongeza hofu kwa wananchi.

Akizungumzia mkutano huo wa pili wenye lengo la kuhakikisha kuwa Afrika inakuwa na umeme kwa miaka ya karibuni alisema mkutano huo una tija ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati hadi ifikapo 2025.

Waziri Muhongo alisema jitihada za Serikali ni kuvutia wawekezaji zaidi kwani kutopatikana kwa waekezaji itakuwa vigumu kwa huduma ya umeme kuwafikia wananchi kutokana na bajeti ya serikali labda  baada ya miaka 200.

Alisema malengo ya kuvutia wawekezaji kutoka nje yamejikita katika kuongeza upatikanaji wa umeme Barani Afrika, kuongeza watumiaji umeme Barani Afrika na uboreshaji wa miundombinu Afrika.

Waziri Muhongo alisema Wizara yake iliahidi hadi kufikia mwakani asilimia 30 ya watanzania watakuwa na umeme jambo ambalo wamefanikiwa hadi sasa ambapo asilimia 36 ya Watanzania wameshapata umeme.

Alisema mikakati yao ni kuhakisha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka ujao asilimia 45 hadi 50 ya Watanzania watakuwa wanatumia huduma ya umeme ambapo mafanikio hayo yatazingatia kasi ya uwekezaji kupitia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme.

Profesa Muhongo alisema iwapo Watanzania watapata huduma ya umeme ni dhahiri kuwa maendeleo yatapatikana kwa haraka hivyo kuendeleza nchi na wananchi wake.


Kwa upande mwingine Waziri Muhongo alisema Serikali kupitia Wizara yake imekuwa ikifanya juhudi za kuhakikisha kuwa vijana Wakitanzania wanapata elimu ya mafuta na gesi katika nchi za nje na ndani ya nchi ili waweze kusaidia katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa rasilimali hizo.

"Hadi sasa tumepeleka vijana kusomea shahada ya uzamili nchini Brazili, Uingereza, China, Norway na wengine wanasoma hapa ambapo malengo yetu ni kwa kipindi cha miaka mitano ijayo tuwe na wasomi wa masuala hayo wafikie 500," alisema Muhongo.

Alisema juhudi hizo zimejikita katika kuhakikisha kuwa kwa kipindi cha miaka kumi ijayo Watanzania asilimia 75 wawe wanapata huduma ya umeme kwa uhakika.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI