UMUIYA YA WAZAZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA WAKE


 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Daftari la wanachama wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Anautoglo. Anayeshuhudia kulia ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed (kushoto) na Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje wakionesha daftari hilo baada ya kuzinduliwa.

 Viongozi wa meza kuu wakipiga makofi wakati wakiimba wimbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kabla ya kuzindua daftari hilo. Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mavela, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu,Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje ,  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed, Katibu wa Elimu na Malezi Taifa, Masoud Bwire na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Dar es Salaam, Nicolaus Msemo.
 Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
  Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kushoto), akiteta jamba na wajumbe wa kamati ndogondogo zilizoundwa ili kurahisisha utendaji kazi wa jumuia hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu na Angelina Malembeka.
 Wajumbe wa Kamati ya Afya, Maafa na Mangira wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto ni Ali Said, Josephat Kadiya na Dk. Meshack Sabaya.

 Wajumbe  wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto ni Omar Njate, Seleman Kumchaya na Seleman Nduda.
Wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Mapambo na Makazi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Janeth Sondoka, Amina Mlewa na Khadija Kingi.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Fedha na Mipango, wakifuatilia uzinduzi huo.
Wajumbe wa Kamati ya Elimu na Malezi wakifurahia jambo. Kutoka kulia ni Amina Mtemvu, Levocatus Machage, Maria Ernesti na Galila Ramadhan.
Wajumbe wakiwa katika uzinduzi huo.

Dotto Mwaibale

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed amewata viongozi wa jumuia hiyo kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.

Mwoto huo aliutoa wakati akizindua Daftari la Wanachama wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam leo.

"Nawapongezeni kwa kuunda kamati ndogondogo ndani ya jumuia itasaidia kusogeza huduma kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla hivyo kukifanya chama chetu kiendelee kuaminiwa" alisema Mohamed.

Alisema tunarasimali kubwa ni vizuri sasa tukazitumia rasimali hizo kukuza uchumi wa jumuia yetu na msipende kusubiri kila kitu muelekezwe na viiongozi wa juu.

JUMUIYA YA WAZAZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA WAKE Alisema kwa mfano katika shule ya jumuia hiyo ya Boza iliyopo mkoani Tanga kuwa ina ardhi ya kutoka lakini haifanyiwi uzarishaji mali wowote.

Mohamed alipongeza Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha daftari hilo kwani litasaidia kuwatambua wanachama wao kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa hivyo kurahisisha shughuli za kisiasa kwa kutambuana katika chaguzi mbalimbali na shughuli za maendeleo.

Katika hatua nyingine Mohamed alisema wanajumuia wote ya wazazi wanaiunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalumu na kuwa wao wanautaka muundo wa serikali mbili kwani ndio utalipeleka mbele Taifa la Tanzania. 

Alitoa mwito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi za mashina wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.

Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia hiyo kiutendaji badala ya kuegemea katika eneo moja la siasa.

"Hii jumuia yetu kwa muda mrefu ilikuwa nyuma kimaendeleo lakini tumedhamiria kuibadilisha na kuwa ya kiutendaji zaidi na ndio maanna tumeanzisha kamati ndogo ndogo za maendeleo na kuwateua watu wenye sifa za kuziongoza yaani wenye taaluma" alisema Cholage


Cholage aliwataka viongozi wote waliochaguliwa kujitambua kuwa wamechaguliwa si kwa bahati mbaya bali ni kwa ajili ya kuleta maendeleo ndani ya jumuia hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI