CCM YAWASAMBARATISHA UKAWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, YAZOA MAELFU YA VITI BILA KUPIGWA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, jana jioni
Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Wananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Nape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo
Lwiza Mbutu akiongoza bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza baada ya kuwasili Nape kwe ye mkutano huo
Twanga akionyesha uhodari wa kuchezambele ya mza kuu
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa
 Kada wa CCM Haji Manara  akiwasalimu wakazi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo. wa  kufunga kampeni za uchaguzi wa  serikali za mitaa uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa jimbo la  Ilala ni sehemu salama sana kwa CCM kwa kuwa jimbo hilo lina historia ya CCM
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa  kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa jimbo la ilala uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Azani Zungu akilonga jukwaani, ambapo aliwataka watendaji wa serikali kuacha kuwabunghudhi mamalishe wa jimbo hilo kwa kuwa ni eneo la biashara tu, hivyo watendaji hao watengeneze mazingira mazuri badala ya timua timua ya mara kwa mara
Nape akihutubia kwenye mkutano huo
Nape akihutubia wananchi kwenye mkutano huo na ifuatayo ni habari kamili ya alichosema
CCM YAWASAMBARATISHA UKAWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Yazoa maelfu ya viti bila kupingwa

Na Bashir Nkoromo
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa.

Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo,
katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.

Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi.

Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji mkubwa  wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi uliopita mwaka 2009.

"Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa CCM iliibuka na ushindi wa asilimia 96, sasa kutokana na dalili za mapema, uchaguzi wa safari hii sina shaka kabisa kwamba wapinzani tutawapiga kwa ushindi wa asilimia mia moja", alisema Nape.

Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo
wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa
kuibuka na ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi.

"Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema Nape.

Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura.

"Nasema bila kificho, vijana wa CCM kama mtamuona mtu yeyote anajaribu kufanya fujo wakati wa upigaji kura mshughulikieni kidogo kabla ya kumpeleka polisi, maana watu wa aina hii wanabaka demokrasia, lazima waadabishwe". alisema Nape na kuongeza.

"Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge unyonge huu hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi fujo na si wa kwanza kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM alishasema kwamba unyonge basi. Sasa mimi hapa napigilia msumari tu".

Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri.

Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga.

Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na  si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.

Katika mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo, Gungu Tambaza.

...Sasa endelea na picha zaidi za mkutano huo
Nape akimkaribisha jukwaani Gungu Mohamed Tambaza, mgombea wa Uenyekiti mtaa wa Mtambani B ili kuomba kura kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa uliofanyika leo  kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
Nape akimsikiliza Gungu Mohamed Tambaza akiomba kura
Kada wa CCM Khamis Mkotya akimpongeza Nape wakati wa mkutano huo
Nape akimpongeza Haji Manara 
Mkotya na Zungu
Mkotya na makada wengine wa CCM wakifuatilia
Shamrashamra uwanjani baada ya mkutano. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI